Katika mwezi july uliomalizaka TRA imekusanya sh.1.055 trion sawa na asilimia 95%.soma zaid
aada ya bunge la bajeti kumalizika hivi karibuni
ambapo Serikali katika mwaka wa fedha
2016/2017 inapanga kutumia jumla ya shilingi
trilioni 29.54 kwa matumizi ya kawaida na
maendeleo.
Shughuli ya makusanyo ya mwaka mpya wa
fedha imeanza ambapo leo August 5 2016
Mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA’ imetoa
taarifa kwamba imekusanya kiasi cha trilioni
1.055 sawa na asilimia 95 kwa kipindi cha July
2016. Katika mwaka huu wa fedha TRA imepewa
lengo la kukusanya shillingi trilioni 15.1
ikilinganishwa na lengo la trilioni 13.32 kwa
mwaka ulioisha.
Akizungumza na waandishi wa habari,
mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi,
Richard Kayombo amesema TRA imeboresha
zaidi mifumo yake ili kupunguza kabisa
changamoto za kutopatikana kwa mtandao
ambayo mara nyingi huathiri makusanyo sasa
wameunganisha mifumo ya TRA na mamlaka ya
bandari Tanzania ilikuhakikisha mapato yote ya
serikali yanakusanywa kwa wakati na usahihi.
TRA imezidi kukumbushia kudai risiti unaponunua
bidhaa na kutoa risiti unapuuza bidhaa ambapo
wamesema kwamba kutotoa risiti na kutodai risiti
ni makosa kwa mujibu wa sheria na hatua za
kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika
kutotoa risiti na kudai risiti.
0 comments :
Post a Comment