Breaking News
Loading...

Advert

Friday, August 5, 2016

Halmashauri ya mufindi mkoani iringa wamefanikiwa kukusanya mapato sh.4.7 sawa na asilimia 82.7soma zaid

Halmashauri ya wilaya ya Mufundi
Mkoani Iringa imefanikiwa kutekeleza
agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania katika ukusanyaji
wa mapato ya ndani, baada ya kukusanya
zaidi ya Shilingi Bilioni 4.7 sawa na
asilimia 82.7 kati ya bilioni 5.6 ilizopanga
kukusanya katika mwaka wa Fedha
2015-2016.
Taarifa ya kitengo cha habari na
mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi, imetanabaisha kuwa, mafanikio
hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa
halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh.
FESTO MGINA kwenye kikao cha kawaida
cha baraza la madiwani wa halmashauri
hiyo kilichoketi mjini Mafinga.
MGINA amesema, mafanikio hayo ni
matokeo ya ufuatiliaji na usimamizi mzuri
wa vyanzo vya mapato vya halmashauri
kama vile mapato yatokanayo na
usafirishaji wa mbao na Magogo, kuuzwa
kwa sehemu ya msitu wa halmashauri
sanjari na ushuru unaokusanywa kwa
wafanyabiashara wadogo katika
halmashauri hiyo.
Aidha, Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa,
pamoja na kutekeleza agizo la Waziri
Mkuu la kila halmashauri kukusanya
mapato kwa asilimia 80 na kuendelea,
kikwazo kikubwa cha kutofikia asilimia
100 ni kuzaliwa kwa halmashauri ya mji
wa Mafinga jambo amabalo lilisababisha
kugawana vyanzo vya mapato .
Mgina, ametaja mkakati wa kufidia
vyanzo hivyo kwa mwaka mpya wa Fedha
2016-2017 kuwa ni pamoja na kuanzisha
stendi katika miji midogo ya Igowole na
Nyololo, kuimarisha doria nyakati za
usiku kwa wafanyabishara wanaotumia
njia za panya kusafirisha mbao na Magogo
hususani nyakati za usiku sanjari na
kuongeza vizuio katika vijiji.
Madiwani katika kikao cha baraza
wakifuatilia kwa umakini.
Mkururugenzi mtendaji wa Halmashauri
Dk. Riziki Shemdoe, akizungumza kama
katibu wa kikao cha baraza.
Mwenyekiti wa halmashauri, Festo Mgina
akizungumzia mafanikio ya ukusanyaji wa
mapato.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top