Yusufu manji akabidhiwa klabu ya Yanga aiendeshe kama klabu binafsi.soma zaid
Wanachama Yanga wamkabidhi Yusuf
Manji aiendeshe Yanga kama klabu
binafsi, mikataba ya kumkabidhi nembo
kusimamiwa na Baraza la Wadhamini.
Katika mkutano huo unaofanyika kwenye
Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam kipindi hiki, Manji amesema
amepeleka ombi la kuikodisha Yanga kwa
miaka 10.
“Nitaikodisha kwa asilimia 75 na 25
inabaki kwa wanachama. Nataka
kuikodisha timu na nembo, majengo ya
klabu yanabaki kuwa mali ya wanachama.
“Katika miaka 10, ikipatikana faida 25
inakwenda kwa wanachama na klabu na
75 kwangu. Kama itakuwa ni hasara basi
inakuwa hasara yangu, hakuna hasara
upande wa wanachama au klabu,”
alisema.
Manji amesema masuala ya timu kuhusu
usajili, mishahara, uendeshaji kama safari
na gharama nyingine zitakuwa chini yake
Wakati huo huo, Wajumbe watatu wa
Kamati Utendaji ya Yanga Ayoub Nyenzi,
Hashim Abdallah na Salum Mkemi
wavuliwa uanachama wa klabu hiyo.
0 comments :
Post a Comment