Mkakati wa serikali ni kuhakikisha unaondoa msongamano wa magari jijini Dar.soma zaid
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano , Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa amesema serikali imejipanga
kuhakikisha wananchi wanakuwa na
usafiri wa uhakika katika kuondoa
msongamano wa magari mijini kwa
Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati
wa uzinduzi wa gari moshi litalofanya
safari zake kuanzia Stesheni ya Dar es
salaam hadi Pugu. Amessema kuwa
kuanza kwa usafiri huo umepunguza
daladala 45.
Amesema kuwa serikali inaendelea na
mchakato wa kuhakikisha inapungaza
kama sio kumaliza kabisa msongamano
wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Profesa Mbarawa amesema kuwa katika
hatua nyingine wanaangalia usafiri kwa
njia ya boti katika baadhi ya maeneo na
wataalam walishafanya kazi hiyo.
Aidha amewataka wafanya kazi kuacha
kufanya kazi kwa mazoea kama
walivyokuwa wakifanya na watakaofanya
hivyo hawatavumiliwa ikiwa ni pamoja na
kufisadi mali za reli.
Hata hivyo amesema waliojenga katika
miundombinu ya reli wanatakiwa
kubomolewa kwani kuwepo kwa nyumba
hizo katika miundombinu hiyo ni kosa
kisheria .Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda amesema wakazi
wa Dar es Salaam kuwa wataondokana na
foleni kutokana na jitihada mbalimbali.
Amesema moja jitihada hizo ni kuondoa
malori ya mafuta ambapo mafuta
yatasafirishwa kwa njia ya bomba mpaka
Chalinze na kuanza kwa safari ya
mikoani. Meya wa Jiji, Isaya Mwita
amewataka wananchi kutumia usafiri huo
kutokana na kutokwa na foleni na
gharama yake kuwa nafuu.
Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja
Kadogosa amesema kuwa kwa usafiri huo
wameanza kutokana na nguvu ya serikali
kuwa karibu katika utoaji wa huduma ya
usafiri huo.
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa akizinduwa safari za gari moshi
leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa na Meya wa Jiji la Dar es
Salaam, Isaya Mwita wakiwa katika
usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari
zake zimezinduliwa leo jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa akipanda katika gari moshi
ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini
Dar es
Salaam.
Wananchi wakiwa katika usafiri wa gari
moshi uliozinduliwa leo jijini Dar es
Salaam.
0 comments :
Post a Comment