Kocha mkuu wa klabu ya Al Ahly ya Misri amejiuzulu kuifundisha klabu hiyo.soma zaid
Kocha mkuu wa klabu ya Al Ahly ya Misri
amejiuzulu chini ya mwaka mmoja baada ya
kuteuliwa kuongoza klabu hiyo.
Mholanzi Martin Jol amejizulu baada ya
kuhudumu kwa miezi sita pekee akisema
anahofia usalama wake.
Mashabiki wa klabu hiyo walionekana kukerwa
sana na kushindwa kwa timu hiyo kufika hatua ya
nusufainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Jol alijibizana na mashabiki Ijumaa iliyopita
baada ya timu yake kutoka sare 2-2 na klabu ya
Zesco United na kuzima matumaini yao ya
kusonga mbele.
Tangu wakati huo amepokea vitisho pia kupitia
mitandao ya kijamii jambo ambalo anasema
limechangia uamuzi wake wa kuondoka.
Source: BBC
0 comments :
Post a Comment