BASATA yatoa Salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Msanii Shakila Said.soma zai
BASATA Yatoa Salamu Za Rambirambi
Kufuatia Kifo Cha Msanii Shakila
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea
kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha
Msanii wa muziki wa taarab Bi. Shakila Said
kilichotokea ghafla nyumbani kwao Mbagala
jijini Dar es Salaam jana Ijumaa ya tarehe
19/08/2016.
Shakila ni msanii na mdau wa muda mrefu wa
sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa na mchango
mkubwa katika kukuza muziki wa taarab nchini
hasa katika kubuni kazi za Sanaa za muziki
mbalimbali ambazo zilikuja kupata umaarufu
mkubwa. Moja ya kazi alizobuni na kupata
umaarufu mkubwa ni pamoja na 'Macho
yanacheka' na 'kifo cha mahaba'.
Mchango wake katika muziki wa taarab hasa
katika kubuni na kutunga nyimbo zenye ubora,
ujumbe na maadili kwa jamii hautasahaulika
kamwe. Ni mwanamuziki aliyeacha misingi
katika sekta ya muziki na alijitolea kwa kiasi
kikubwa katika kuufikisha muziki wa taarab
mahali ulipo leo.
Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa
hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote
aliyotuachia marehemu Shakila hasa katika
kupenda kujitolea muda mwingi katika kukuza
muziki wa taarab na sekta ya muziki kwa
ujumla.
Baraza linatoa pole kwa ndugu wa marehemu,
shirikisho la muziki, wasanii na wadau wote wa
Sanaa katika kipindi hiki kigumu cha
kuondokewa na mpendwa wetu.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen
0 comments :
Post a Comment