Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 17, 2016

Majambazi 2 wameuwawa kwa kupigwa risasi mkoani kilimanjaro.

Watu wawili wanaosadiki ni majambazi sugu
wameuawa kwa kupigwa risasi mkoani
Kilimanjaro baada ya kuhusishwa kwenye
matukio kumi na moja ya unyanganyi wa kutumia
silaha na mauaji katika mikoa ya Arusha,
Kilimanjaro, Mbeya na nchi jirani ya Kenya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro
Bw.Wilbroad Mutafungwa amesema watuhumiwa
hao wameuawa baada ya kufanya jaribio la
kutoroka askari polisi wakati walipoenda
kuwaonyesha mahali walipoficha silaha aina ya
bastola moja na shortgu katika maeneo ya Kahe.
Amesema makachero wa jeshi la polisi
walilazimika kuwafyatulia risasi kuwaelekezea
miguuni lakini kwa bahati mbaya mmoja risasi
ilimpata ya mgongoni na mwingine kiunoni na
kwamba walifariki dunia wakati wakikimbizwa
katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro
Mawenzi.
Katika tukio lingine jeshi la polisi mkoa wa
Kilimanjaro linawashikilia watu watano wakiwemo
wanawake wawili kwa tuhuma za kumua kikatili
mwanamke Neema Ndewera mkazi wa Mbokomu
kwa kumchoma kisu shingoni na masikioni na
kutupa mwili wake chooni.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top