Walimu wakuu shule 68 wa shule za msingi watakiwa kuvuliwa vyeo.
WALIMU wakuu wa shule 68 wa shule za Msingi
wanatakiwa kuvuliwa na kunyang'anywa vyeo
vyao kwa kosa la udananyifu wa takwimu za
wanafunzi hewa tangu elimu itangazwe kuwa
bure.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Ally Salum Hapi wakati akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo.
Amesema kuwa walimu wakuu hao wametakiwa
kuvuliwa vyeo vyao na kuwapa walimu wengine
kwa kosa la kutoa takwimu za wanafunzi hewa
3462 wa shule za msingi 68 za Wilaya ya
Kinondoni. Pia hatua kali za Kisheria
zitachukuliwa kwa dhidi ya walimu wakuu wa
shule hizo.
Pia Hapi amemwomba Katibu Tawala wa Mkoa
kuwavua vyeo wakuu wa shule 22 wa shule za
Sekondari 22 za Manispaa ya Kinondoni na
Ubungo kwa kosa la kutoa takwimu za uongo na
kuweka wanafunzi hewa.
Wakuu wa shule za Msingi hao wamekuwa na
wanafunzi hewa 2534 kutoka shule 22 za
Sekondari za Manispaa ya Kinondoni na
Manispaa ya Ubungo.
Wakuu wa shule hizo wameisababishia Serikali
kupoteza zaidi ya shilingi milioni 60 kwa
kupeleka fedha za kuwahudumia wanafunzi
wanaosoma katika shule hizo.
Baadhi ya shule za sekondari zilizokutwa na
wanafunzi hewa ni Boko wanafunzi 74, Bunju
B155, Goba Mpakani 42 na Hananansifu
wanafunzi 154. Na shule za Sekondari ni Msisiri
B wanafunzi hewa 395, Upendo 273 na Ubungo
Msewe 267.
0 comments :
Post a Comment