Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 17, 2016

Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Ulaya amekamatwa na polisi.soma zaid

Zikiwa zimeshalia siku chache kabla ya
kualizika kwa mashindano ya Olimpili 2016
inayofanyika Rio, polisi nchini Brazil
wamemkamata Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya
Ulaya, Patrick Hickey kwa kosa la kuuza tiketi
kinyume na makubaliano.
Inaripotiwa kuwa Hickey alikamatwa na Polisi
baada ya kugundulika kuwa alikuwa akiuza tiketi
za Olimpiki kwa gharama kubwa tofauti na bei
inayotakiwa.
Katika taarifa ambayo imetolewa na Polisi wa
nchi hiyo inaeleza kuwa wakati wakitaka
kumkamata mtu Hickey alijaribu kuwatoroka
lakini walifanikiwa kumkamata wakati alipotaka
kuwakimbia kutoka katika chumba chake na
kuhamia chumba kingine cha hoteli.
Hata hivyo vyombo vya habari vya Brazil
vinaamini kuwa sababu ya kukamatwa Hickey
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Olimpiki
la Irenland (OCI) inahusiana na MuIreland
mwenzake, Kebin James Mallon ambaye alitiwa
mbaroni na Polisi siku ya ufunguzi wa michezo
hiyo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top