Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 17, 2016

Serikali kuhakiki matamko ya mali za vigogo 500.soma zaid

WAKATI takribani asilimia 20 ya viongozi wa
umma kwa mwaka 2011 hadi mwaka jana
hawakuwasilisha matamko ya mali zao kwa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
kwa wakati, mwaka huu serikali imetangaza
kuhakiki matamko ya mali za viongozi 500.
Aidha, serikali hiyo imebainisha wazi kuwa
haitowafumbia macho viongozi,
watakaoshindwa kuwasilisha matamko ya mali
zao kwa mujibu wa sheria, ikiwemo viongozi
watakaowasilisha matamko ya mali
yatakayobainika kuwa na udanganyifu.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Angella Kairuki wakati akifungua
warsha ya wadau, kujadili taarifa ya matokeo ya
utafiti kuhusu hali ya maadili nchini Dar es
Salaam jana.
Kairuki alikiri kuwa hata katika tafiti nyingine
ndogo, zilizofanyika kuhusu hali ya maadili
nchini pamoja na takwimu kubadilikabadilika,
lakini zilibainisha kuwepo kwa viongozi
wasiowasilisha matamko yao ya mali na
wengine kutowasilisha kwa wakati.
Alisema taarifa hiyo ya utafiti kuhusu hali ya
maadili ya viongozi nchini kwa miaka mitano
kuanzia 2011 hadi mwaka jana, ilibainisha kuwa
pamoja na kuwepo kwa mwamko wa viongozi
kuhusu suala zima la maadili, bado asilimia 20
ya viongozi hao wa umma hawakuwasilisha
matamko yao ya mali kwa wakati.
“Tumepokea taarifa hii na imetutia hamasa kwa
kweli, tumeona asilimia 20 hawarejeshi kwa
wakati matamko yao, hawa ni wengi sana
ikizingatiwa kuwa ni viongozi, tunatoa onyo
hakuna atakayefumbiwa macho endapo atakiuka
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kwani
atachukuliwa hatua stahiki za kisheria,” alisisitiza.
Alisema kwa kawaida endapo kiongozi
asipowasilisha tamko la mali zake hadi ifikapo
Desemba 31, huhojiwa na Baraza la Maadili ya
Viongozi wa Umma, lakini pia inapothibitika
kuwa alikiuka kwa makusudi sheria hiyo ya
maadili ya viongozi huchukuliwa hatua za
kisheria.
Alisema mwaka huu, kuna jumla ya viongozi wa
umma 15,624 kati ya hao viongozi 500 tayari
wameshatengewa fedha kwa ajili ya mali zao
kuhakikiwa na endapo fedha zitapatikana idadi
hiyo inaweza kuongezeka na kufikia 1,000.
“Miaka ya nyuma tulikuwa tunahakiki kwa mwaka
viongozi 100 hadi 200, safari hii tumejipanga
kuanza na viongozi 500. Lakini katika hili
tunaomba wananchi nao watusaidie kuhakiki mali
za viongozi hawa wa umma kwani sheria inawa
ruhusu kufanya hivyo, ili kuweza kubaini viongozi
wadanganyifu,” alisema.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA),
Profesa Kessy aliyefanya utafiti huo kwa
kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi, alisema lengo la utafiti huo ni
kuangalia hali halisi ya maadili nchini kuanzia
viongozi hadi kwa wananchi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top