Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, August 18, 2016

Tundu Lissu ameonesha unahiri wake katika sheria baada ya kutumia dk120 mahakani.soma zaid

Tundu Lissu, ambaye ni wakili wa Mbunge wa
Bunda Mjini, Ester Bulaya jana alitumia muda
wa saa mbili kupangua maombi ya wananchi
wanne wanaopinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu
yaliyompa ushindi mteja wake.
Kesi hiyo imeanza kusikilizwa tena baada ya
Mahakama ya Rufaa kufuta uamuzi wa
Mahakama Kuu uliotupilia mbali hoja za kupinga
matokeo hayo, ambazo ziliwasilishwa na
wafuasi wanne wa aliyekuwa mgombea wa
jimbo hilo, Steven Wasira (CCM).
Jaji Mohamed Gwae wa Mahakama Kuu,
alitupilia mbali kesi hiyo baada ya kukubali
pingamizi la Lissu kuwa wafuasi hao hawakuwa
na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo.
Wakazi hao wa Bunda wanadai kuwa uchaguzi
haukuwa huru na haki kutokana na kugubikwa
na vitendo vya rushwa, mgombea
wanayemuunga mkono kunyimwa fursa ya
kuhakiki matokeo na pia kuongezeka kwa idadi
ya vituo vya kupigia kura.
Jana, Lissu, ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa
Chadema na wakili wa kujitegemea, alitoa
majibu ya utetezi mbele ya Jaji Lameck Mlacha
kuanzia saa 4.10 asubuhi na kukamilisha saa
6.02 mchana wakati shauri hilo lilipoahirishwa
kwa muda hadi saa 8:00 mchana kutoa fursa
kwa mawakili wa upande wa wadai, Constantine
Mutalemwa kujibu.
Lissu alidai kuwa waleta maombi wameshindwa
kutoa hoja mahususi kuonyesha ukiukwaji wa
sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi
wanazodai ulikuwepo katika mchakato wa
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.
Wakili Lissu pia alidai kuwa walalamikaji ambao
ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes
Ezekiel na Ascetic Malegele, pia wameshindwa
kuonyesha madhara waliyopata kama
wapigakura kuishawishi mahakama kutengua
matokeo yaliyompa ushindi Bulaya dhidi ya
mwanasiasa huyo mkongwe.
“Waleta maombi wanadai uchaguzi haukuwa huru
na haki, idadi ya wapigakura kutofautiana kwa kila
kituo na uwepo wa vitendo vya rushwa, lakini
hawabainishi wazi nani mhusika wa mambo
wanayoyalalamikia na madhara waliyopata kwa
nafasi yao ya wapigakura,” alisema wakili Lissu.
Alisema vitendo vya rushwa katika uchaguzi ni
kosa kubwa linaloweza kusababisha
kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi mzima,
lakini walalamikaji wana wajibu wa kumtaja
mhusika wa vitendo hivyo ili kuipa mahakama
fursa ya kutafsiri vyema sheria na kutoa haki.
“Lakini madai ya juujuu tena ya jumla kuwa
aliyetoa rushwa ni wakala wa mteja wangu,
hayakubaliki mbele ya macho ya sheria kwa
sababu mtu huyo hajulikani na jukumu la
kuthibitisha madai ni la mleta maombi na
uthibitisho huo haumo kwenye hati yao ya
maombi,” alidai Lissu.
Aliomba maombi hayo yafutwe kwa hoja
kwamba wadai hawajataja vifungu vinavyoipa
mahakama haki na mamlaka ya kuyasikiliza na
kuyaamua.chanzo mpekuzi blog

0 comments :

Post a Comment

Back To Top