Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, August 16, 2016

Serikali imelazimika kusitisha fedha kwa wanafunzi wa vitendo kwa wiki mbili.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
Prof Joyce Ndalichako amesema wizara hiyo
imelazimika kusitisha malipo ya fedha za
mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa elimu
ya juu kwa muda wa wiki mbili ili kupisha zoezi
la uhakiki wa wanafunzi hewa
Amesema hadi sasa wanafunzi hewa zaidi ya
2000 tayari wamebainika kwenye vyuo
mbalimbali nchini na walikuwa tayari kupokea
fedha hizo jambo ambalo ni hasara kwa serikali.
Prof. Ndalichako amesema, tayari amewaagiza
wakuu wote wa vyuo kuwasilisha upya majina
ya wanafunzi wanaostahili kupatiwa fedha hizo
bila udanganyifu.
Amefafanua kwamba, wamegundua taarifa
zilizopelekwa awali zilikuwa na udanganyifu
hivyo serikali imelazimika kusitisha zoezi la
upelekaji fedha kwenye vyuo hivyo.
Kwa upande wa wanafunzi ambao vyuo vyao
vimefungiwa Prof. Ndalichako amesema tayari
wametoa maelekezo ya kuwasaidia kupata haki
yao muhimu ya kusoma na kusisitiza hakuna
mwanafunzi hata mmoja ambaye atakosa
msaada wa serikali

0 comments :

Post a Comment

Back To Top