Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 10, 2016

Marufuku kuwabambikizia kesi raia wema kwa maslahi binafsi.soma zaid

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu
Nchemba amewaambia askari wa jeshi la Polisi
mkoani Katavi kufanya kazi kwa taratibu na
sheria bila kumuonea mtu yeyote hasa
wanyonge.
Waziri Mwigulu ametoa agizo hilo wakati wa
ziara yake ya kutembelea makazi ya watanzania
wapya pamoja na kuzungumza na askari wa
jeshi la polisi, Magereza pamoja na Uhamiaji.
Mhe. Mwigulu amesema kuwa Askari hao
waondokane na tabia ya matukio ya
kuwabambikizia kesi raia kwa maslahi binafsi na
kuwaonea na kusema kuwa serikali kali ya
awamu ya tano haitamfumbia macho askari
atakayebainika kufanya hivyo.
Aidha Waziri Mwigulu amechukua fursa hiyo
kuwapa hamasa Askari hao kwa kusema kuwa
serikali itawaboreshea maslahi yao kadri bajeti
itakavyoruhusu ili waweze kufanya kazi kwa
weledi zaidi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top