Mkazi mmoja Arusha amefutiwa kifungo cha miaka 30 jela.soma zaid
Arusha. Mahakama ya Rufani imemfutia adhabu
ya kifungo cha miaka 30 jela, Johnson Ashraf
mkazi wa Mererani, ambaye alikuwa amefungwa
kwa kosa na ujambazi wa kutumia silaha.
Ashraf alitiwa hatiani na Mahakama Kuu Kanda
ya Arusha baada ya kutuhumiwa Mei 31 mwaka
2005, akiwa na wenzake saa tisa usiku
walivunja nyumba na kuiba vitu vyenye thamani
ya Sh 8.1 milioni mali ya Dismas John kwa
kutumia silaha.
Majaji watatu wa mahakama ya rufani, Jaji
Edward Rutakangwa, Jaji Angela Kileo na Jaji
Salum Masati walitoa maamuzi hayo baada ya
kupitia rufani ya mtuhumiwa huyo na ushahidi
wa pande zote.
0 comments :
Post a Comment