Vyuo vya nje viko tayari kupokea vijana wenye ufaulu wa G.P.A 2.5.soma zai.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Global Link Education, Abdumaliki Mollel
amesema hayo leo jijini Dar, kuwa vyuo
vya nje viko tayari kupokea vijana wenye
sifa hizo.
Mollel amesema kuwa vijana wasikate
tamaa Global Link Education iko kwa ajili
ya yao katika kuhakikisha ndoto zao
hazipotei kutokana na kukosa nafasi
katika vyuo vya ndani
Amesema kuwa wazazi waache kuogopa
gharama za kusoma vyuo vya nje kwani
gharama za kusoma nje ni sawa na vyuo
vya ndani hivyo vijana watumie furssa
hizo.
Mollel amesema ndani ya nchi
mwanafunzi anachukuliwa kujiunga na
elimu ya juu kwa sifa kuanzia alama D
sawa pointi 4 kama mfumo mpya wa Tume
ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) na mfumo huo
ndio utakaotuumika kwa mtu yeyote
kwnda kusoma nje ya nchi
Amesema wazazi na wanafunzi
wanachanganywa na mfumo huo na
kutaka kuacha kutishika kutokana kuwa
uwezo wao kusoma nje bado wanao.
Aidha amesema kuwa global link
education inawaka vijana na wazazi
kuchangamkia fursa zilizopo katika
kusoma nje na mazingira ya vyuo hivyo
vina uwezo naa ubora katika utoaji wa
elimu katika fani mbalimbali.
Amesema kuwa wanafunzi kuwa kuna
watu wamesoma masomo ya sayansi lakini
kutokana vyuo vya udaktari kuwa
vichache wanakosa nafasi hivyo
wanashindwa kufurahi na masomo hayo
ktika kuwaaletea matunda.
0 comments :
Post a Comment