Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 10, 2016

Timu ya Mo Bajaia kutoka Algeria imetua Jijin Dar kwa ajili ya mechi dhidi ya Yanga Agost 13.soms zaid.

JUMLA ya kikosi cha watu 35 ambao ni
wachezaji na viongozi wa MO Bajaia
kutoka Algeria, wametua Dar es Salaam,
usiku wa kuamkia Agosti 9, 2016 na
imefikia Hoteli ya Ledger Plaza, iliyoko
Kunduchi Beach nje kidogo ya jiji la Dar
es Salaam.
Timu hiyo imekuja kucheza na Young
Africans ya Dar es Salaam, katika mchezo
wa nne wa hatua ya Nane Bora kuwania
Kombe la Shirikisho Barani Afrika
utakaofanyika Jumamosi Agosti 13, 2016
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Licha ya kwamba Young Africans kuwa na
pointi moja, bado ina nafasi ya kushika
nafasi za juu katika kundi la A ambalo
msimamo wake unaongozwa na TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC), huku Mo Bajaia ya Algeria
na Medeama ya Ghana, zina pointi tano
kila moja. Wakati Young Africans
wanacheza na Mo Bajaia iliyoshinda
mchezo wa kwanza huko Algeria,
Medeama itakipiga na TP Mazembe.
Mchezo wa Young Africans dhidi ya Mo
Bajaia utachezeshwa na waamuzi kutoka
Ethiopia ambako katikati atakuwa Bamlak
Tessema Weyesa akisaidiwa na Kindie
Mussie mstari upande wa kusini na
Temesgin Samuel Atango katika mstari wa
Kaskazini upande wa wakati Mwamuzi wa
Akiba atakuwa Haileyesus Bezezew Belete.
Kamishna wa mchezo atakuwa Gaspard
Kayijuka kutoka Rwanda wakati Desire
Gahuka wa Burundi atasimamia ufanisi
wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu
wa mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka
Sudan. Mratibu huyo anatarajiwa kuwasili
leo Agosti 10, 2016 wakati waamuzi
watatua kesho Agosti 11, 2016 na
msimamizi wa waamuzi atatua Ijumaa
Agosti 12, 2016.
Kiingilio katika mchezo huo kitakuwa ni
Sh 3,000 kwa mzungunguko kwa maana ya
viti vya kijani, bluu na chungwa wakati
Viti Maalumu vyenye hadhi ya daraja B na
C kiingilio kitakuwa Sh 10,000 wakati A
kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 kwa mujibu
wa Waratibu wa Young Africans

0 comments :

Post a Comment

Back To Top