Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 10, 2016

Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi dunian zinazo wawezesha wanawake.soma zaid

Mfuko wa Hanns Seidel Foundation (HSF)
unaojihusisha na uwezeshaji wa wanawake
katika nyanja za uongozi, usawa kijinsia na
masuala ya siasa katika nchi mbalimbali
umeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi
zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa
wanawake duniani.
Mwenyekiti wa Mfuko huo ambao makao yake
yako nchini Ujerumani Prof. Prof.Ursula Mannle
ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati
hafla fupi iliyoandaliwa na mfuko huo kwa lengo
la kufanya tathmini ya mchango wa HSF nchini
Tanzania katika kuwajengea uwezo wanawake
vijana katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia
na masuala ya siasa.
Prof. Ursula amesema kuwa HSF imekuwa
ikitekeleza program mbalimbali za uwezeshaji
kwa wanawake kisiasa, kuwaandaa na
kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi mahiri
katika nchi wanazotoka.
Amesema HCF imeamua kuanzisha programu
maalumu nchini Tanzania kwa ajili ya
kuwaangalia wanawake wanaojitokeza kugombea
katika nafasi mbalimbali za uongozi ili
kuwawezesha kuwa viongozi katika nafasi
mbalimbali serikalini pia kuziba pengo lililopo la
uwakilishi katika nafasi za kisiasa.
Ameeleza kuwa Hanns Seidel Foundation
itaendelea kuwaunga mkono wanawake wa
Tanzania wanaojitokeza kuwania nafasi
mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania kupitia
program mbalimbali za ufadhili ili kuwawezesha
kumudu gharama na kuwajengea uwezo wa
kushindana katika majukwaa ya Siasa.
Waziri Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Tanzania
Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa
hafla hiyo amesema kuwa Serikali ya Tanzania
imeendelea kutoa kipaumbele katika nafasi za
uongozi kwa wanawake.
Amesema licha ya kuwepo kwa changamoto
mbalimbali zinazowakabili wanawake vijana wa
Kitanzania zikiwemo za kijamii na kimila pia
ndoa na mimba za utotoni zinazochangia vijana
wanafunzi wa kike kuacha masomo yao, Serikali
ya awamu ya Tano imeamua kuja na Sera ya
Elimu bure kuwawezesha vijana wa kike wa
kitanzania kupata elimu.
Amesema Tanzania imeendelea kuwathamini
wanawake katika uteuzi wa ngazi mbalimbali za
uongozi Serikalini kuanzia wakuu wa Wilaya,
Mikoa, Wakurugenzi, Mawaziri na Naibu
Mawaziri pia uwepo wa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan ambaye ni alama ya hamasa na
ushindi katika uongozi kwa wanawake wengine
Tanzania.
Mhe. Mwalimu ameushukuru Mfuko huo kwa
mchango wake katika kuwainua wanawake wa
Tanzania pia program mbalimbali zilizoanzishwa
na mfuko huo kwa lengo la kuwawezesha
wanawake nchini.
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Kazi na
Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie
Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria katika
kushughulikia masuala ya wanawake amesema
kuwa kupitia Sera zinazosimamia masuala ya
wanawake mambo mengi yameweza kufanyika.
Ametoa wito kwa Tanzania kuendelea
kuzishughulikia changamoto mbalimbali ambazo
zimekuwa kikwazo kwa wanawake wa Tanzania
kufika mbali na kuwazuia wasiweze kusimama
wenyewe katika masuala ya Siasa.
Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la
Ilemela Mhe. Angelina Mabula ambaye ni
miongoni mwa wanawake wa Tanzania
walionufaika kutokana na HSF amesema kuwa
alianza harakati za siasa mwaka 2004 licha ya
kuwepo kwa changamoto mbalimbali.
Amesema kuwa ipo haja ya wagombea
wanawake vijana wanaoingia katika ulingo wa
siasa kusaidiwa kifedha na mfuko huo pamoja na
vyama vyao vya siasa wanavyoviwakilisha pindi
wanapogombea nafasi mbalimbali za uongozi na
kuongeza kuwa wakati umefika kwa wanawake
wanaoingia katika siasa kusimama wenyewe
kwenye majimbo ya uchaguzi.
Ametoa wito kwa HSF kuendelea kuwasaidia
wanawake vijana wanaoingia kwa mara ya
kwanza katika masuala ya siasa kwenye chaguzi
zinazokuja ili kuwawekea mazingira mazuri ya
kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top