Matunzo ya vifaranga ya kuku vikiwa vidigo.soma zaid
1. Utayarishaji wa banda.
i. Banda liwe safi, lisafishwe lisiwe na vumbi.
ii. Pulizia dawa ya kuondoa viroboto, utitiri na
chawa kwa kutumia dawa kama Ectomin Dip.
ii. Pulizia dawa ya kudhibiti wadudu
wasababishao magonjwa, tumia disinfectant
mfano Vivid/TH4.
Tayarisha taa na moto (charcoal) kwa ajili ya
kuweka chumba kiwe na joto la kutosha.
SIKU YA 1.
i. Vifaranga wanapofika tu wapewe
Glucose kwenye maji kwa masaa 8 mfululizo.
ii. Baada ya hapo wapewe Vitalyte
kwa siku 2 mfululizo.
SIKU YA 3.
Wapewe chanjo ya Newcastle
Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo
wapatie Vitalyte au Antistress kwa siku 3
mfululizo.
SIKU YA 7.
Wapewe chanjo ya Gumboro
Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo
wapatie maji ya Antistress kwa siku 2 mfululizo.
SIKU YA 10.
Wapatie OTC Plus kwa siku kwa
saa 24 kwa siku 3 mfululizo.
SIKU YA 14/18/19.
Wapatie Esb3 na Vitalyte kwa
masaa 24 kwa siku 3 mfululizo.
SIKU YA 21.
Wanyweshe Newcastle Vaccines
kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie
Antistress kwa siku 4 mfululizo.
SIKU YA 28.
Wapewe Gumboro Vaccines kwa
saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie
Antistress kwa siku 2 mfululizo.
SIKU YA 31.
Wapatie OTC Plus kwa siku 7
mfululizo.
SIKU YA 43/44/45.
Wapatie Esb3 na Vitalyte kwa
masaa 24 mfululizo kwa siku 3.
SIKU YA 50.
Wapewe chanjo ya Fowl Pox. Baada
ya hapo endelea kuwapa Chickmycin au Chick
Plus kwa wiki 2 mfululizo.
SIKU YA 65.
Chanjo ya Gumboro na baada ya
hapo endelea na Antistress.
SIKU YA 69.
Wapatie dawa ya Minyoo mfano
Levalap kwa siku 2 mfululizo.
SIKU YA 72.
Wapewe Fluquin kwa siku 5
mfululizo.
SIKU YA 79.
Wapewe Anticox na Vitalyte kwa
siku 5 mfululizo.
SIKU YA 90.
Wapewe tena chanjo ya Newcastle
Vaccines kwa saa 2 mfululizo.
Baada ya hapo endelea kuwapa Antistress kwa
siku 3 mfululizo.
Hapo sasa endelea na Utaratibu wa kawaida wa
chanjo na tiba.
0 comments :
Post a Comment