BENKI ya CRDB imepunguza kasi ya utoaji mikopo.soma zaid
Dk. Kimei: Hali ya uchumi tete
BENKI ya CRDB imesema imepunguza kasi ya
utoaji mikopo kuangalia hali ya uchumi nchini
inavyokwenda.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi
Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei,
alisema kwa sasa beni hiyo inaangalia ni sekta
ipi yenye mwelekeo wa kukopesheka.
“Kipindi hiki ni cha mpito bado watu hawajatulia,
tunaangalia ni sekta ipi yenye mwelekeo kwa
sababu kama hoteli zinayumbayumba lazima
tusubiri hali ikae vizuri.
“Sisi tunasimamia fedha za watu hivyo hatuwezi
kucheza nazo, tunazidi kujipanga kufuatana na
sera ya Serikali,” alisema Dk. Kimei.
Akitoa mfano, alisema sekta za mafuta na gesi ni
kama vile zimesimama hivyo CRDB inasubiri hali
ikae vizuri iweze kufanya tathmini.
“Mikopo mingine kama ya watu binafsi
tunaendelea kuitoa na kama ni waajiriwa waje
watapewa lakini katika sekta nyingine hali
imekuwa tete sana,” alisema.
Serikali ilieleza kuwa miongoni mwa maeneo ya
vipaumbele yatakayozingatiwa kama
yalivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa
Taifa wa mwaka 2016/17 ni pamoja na
kuendeleza huduma za fedha, biashara na
masoko.
Hata hivyo, hatua ya Serikali kutangaza mkakati
wa kupunguza na kuondoa matumizi yasiyo ya
lazima imeanza kuathiri sekta nyingi ikiwamo ya
fedha.
Lichaya mkakati wa kubana matumizi, pia Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika ada
ambazo benki inatoza wateja wake kwenye
huduma mbalimbali zinazotolewa ni miongoni
mwa vitu vilivyochangia mtikisiko huo.
Wakati akisoma bajeti ya serikali bungeni kwa
mwaka 2016/17, Waziri wa Fedha, Dk. Philip
Mpango, alisema serikali inakusudia kutoza VAT
katika huduma za benki zinazotozwa na benki
zote nchini ili kupanua wigo wa kodi.
0 comments :
Post a Comment