Deni la klabu ya Yanga limefikia sh.5.4Billion.soma zaid
TAARIFA ya mapato na matumizi ya klabu ya
Yanga inaonyesha kwamba deni la klabu hiyo
sasa limefikia Sh 5.4 Bilioni.
Taarifa hiyo kwa mwaka 2016 imeonyesha kuwa
Yanga alikopa kiasi cha Sh 1.5 Bilioni kwa msimu
wa 2015/16 ili kuziba pengo lilijitokeza katika
bajeti yao kitendo ambacho kimefanya deni hilo
lifikie Sh 5.4 Bilioni.
“Kwa miezi 12 tumekuwa na Sh 1.5 Bilioni
ambayo klabu imekopa bila riba, na imekuwa
ikikopa kwa miaka kadhaa na imeshindwa kulipa,”
ilisomeka taarifa hiyo. “Mkopo unatoka kwa
mwanachama mmoja wa timu ambaye hadi sasa
kachangia Sh 1.5 Bilioni na kwa miaka 10 mkopo
umefikia Sh 5.4 Bilioni,’’ilieleza taarifa hiyo.
Pia imebainika kuwa kwa mwezi huu (Agosti)
Yanga itahitaji Sh 500 Milioni kuendesha shughuli
zake mbalimbali, ukiacha Sh 88 milioni
zinazotokana na udhamini wa Kampuni ya
Quality Group.
Licha ya taarifa hiyo kutomtaja mwanachama
anayeidai Yanga, Mwanaspoti inafahamu kuwa ni
Quality Group ndiyo inayotoa mkopo huo kwa
udhamini wake na imekuwa ikifanya hivyo miaka
10 sasa.
Kutokana na kutokuwepo kwa mapato ya
kueleweka Yanga, deni hilo linatarajiwa kuendelea
kukua katika miaka miwili ijayo kwani mpaka
sasa hakuna marejesho yoyote aliyoanza
kufanyika.
Katika mkutano mkuu wa dharura hivi karibuni,
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye
aliwahi kuwa mkurugenzi Quality Group kabla ya
kujitoa aliwataka wanachama wa Yanga kubadili
mfumo wa uendeshaji ili wamkodishie timu na
nembo aiendeshe kwa faida na kuwapa mgao wa
asilimia 25.chanzk mwanaspot
0 comments :
Post a Comment