Msanii Pam D amesema wanaume wengi wanogopa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wasanii wa kike.soma zaid
Msanii wa kike Pam D ambaye kwa sasa
anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Nipe nono’
aliomshirikisha Nay wa Mitego amesema kuwa
baadhi ya wanaume wanaogopa kuwa na
mahusiano ya kimapenzi wasanii wa kike wa
bongo fleva.
Akiongea kwenye E newz PAM amedai kwamba
watu wengi wanawachukulia wasanii wa kike
kama watu wenye mambo mengi na wengine
kuogopa kusalitiwa akijitolea mfano yeye kuwa
anatamani kumpata mtu ambaye atakuwa
serious,lakini mwanaume wengi wamekuwa
wakiogopa.
“ Kwanza kuna baadhi ya wanaume unakuta
wanatuogopa ujue, wanaona labda
tunawadanganya,hawajiamini wenyewe ” alisema
Pam D na kuongeza angepata mwanaume aliye
serious kama Nay wa Mitego angeshukuru sana.
Source: EATV
0 comments :
Post a Comment