January 26, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Monday, August 1, 2016

Adaiwa kujimwagia petrol na kujilipua kutokana wivu wa mapenzi.soma zaid.

MOROGORO: Wivu wa mapenzi? Kigogo mmoja
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani
hapa ambaye ni bosi wa kitengo cha manunuzi,
Jackson Maghembe, anadaiwa kutaka kulipua
nyumba anayoishi mkewe, Cesilia Njuli kisha
kuishia kujilipua mwenyewe.
Cesilia Njuli ambaye ni mke wa Jackson
Maghembe.
Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita Mtaa wa Kilosa
Town Kata ya Mkwatani-Manzese A wilayani
Kilosa baada ya wawili hao kuhudhuria kwenye
shoo ya Mwanamuziki Aisha Ramadhani ‘Isha
Mashauzi’ iliyofanyika katika Ukumbi wa Bablon.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, wakiwa
kwenye shoo hiyo, Maghembe alidaiwa kumpiga
mkewe na baadaye kwenda nyumbani kuunguza
nyumba hiyo kwa petroli huku watoto wao
wawili na mfanyakazi wa ndani wakiwa
usingizini.
Kufuatia ukubwa wa tukio hilo, Wikienda lilifika
nyumbani hapo na kuzungumza na mke wa
jamaa huyo ambaye alisimulia kisa na mkasa:
“Huyu mume wangu nimezaa naye watoto
wawili, mwezi wa nne nilimpeleka polisi kwa
mara ya tatu ambako tulikubaliana tuachane na
tukatiliana saini kwenye jalada lililofunguliwa
namba KL\LR\390\2016.
“Baada ya pale, kila mmoja akawa anaishi
kwenye nyumba yake na mimi nikawa ninaishi
na wanangu.
“Wiki iliyopita nilikwenda kwenye shoo ya
Mashauzi kupoteza mawazo. Nikiwa pale
ukumbini, yule mume wangu alikuja na
kuniomba tucheze wote.
“Kwa kumheshimu kama baba wa watoto
wangu nilikubali. Cha ajabu muziki ulipokwisha
alining’ang’ania nikalale kwake. Nilimkatalia
ndipo akaning’oa wigi kichwani na kunipiga.
“Baada ya kutoka pale ukumbini alikwenda
kununua petroli akaimwaga madirishani kwa
lengo la kuichoma moto nyumba huku wanaye
na msichana wangu wa kazi wakiwa wamelala.
Nyumbani kwa marehemu
“Wakati akimwaga petroli ilimlowanisha nguo
zake hivyo alipowasha kibiriti nyumba iliungua
na moto mwingine ulinasa kwenye nguo zake na
kumuunguza vibaya.
“Majirani walipofika kwa kushirikiana na
mpangaji wangu, Ayoub Paul na msichana
wangu wa kazi, Esther Jonas waliwaondoa
wanangu na kuhangaika kuuzima moto.
“Kwa sasa yupo hoi Hospitali ya Kilosa
kutokana na hali yake kuwa mbaya.”
Hata hivyo, mke huyo ambaye ni nesi wa
Hospitali ya Wilaya ya Kilosa alikwenda
kumfungulia mumewe huyo jalada la kesi namba
KL\ RB\1141\2016 –SHAMBULIO LA KUDHURU
MWILI NA UHARIBIFU WA MALI huku madaktari
wa hospitali hiyo wakieleza kuwa hali ya jamaa
huyo bado ni tete.
Source: Global Publisher

0 comments :

Post a Comment

Back To Top