Breaking News
Loading...

Advert

Monday, August 1, 2016

Rais wa simba Evans Aveva amepatwa na kigugumizi mbele ya wanachama wa simba.soma zaid

KUTANO Mkuu wa Simba ulivunjika jana baada
ya rais wake, Evans Aveva kuzidiwa na hoja ya
wanachama kutaka mfanyabiashara maarufu
nchini, Mohamed Dewji au Mo, akubaliwe
kununua hisa.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye bwalo la
Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam,
wengi wa wanachama hao walitaka kujadili hoja
moja tu ya Mo na zingine ziwekwe kando.
Baada ya kuzidiwa na kelele za wanachama
waliokuwa wakilitaja jina la Mo kila mara, Aveva
aliamua kuizungumzia hoja hiyo, lakini bila kufikia
muafaka aliamua kuvunja mkutano huo.
Alisema kuwa hoja hiyo itafanyiwa kazi na
kuwafanya wanachama kulipuka kwa furaha
wakilitaja kwa nguvu jina la Mo, na hapo ndipo
Aveva alipopata nafasi ya kuuvunja mkutano huo.
Mo alipendekeza auziwe hisa za asilimia 51 kwa
gharama ya Sh bilioni 21 huku zile zilizobaki 49
atawanunulia wanachama wa muda mrefu wa
klabu hiyo ili iendeshwe kikampuni.
Wanachama wa Simba waliushinikiza uongozi
wao kujadili hoja namba tisa iliyohusu Mo
kununua hisa hizo na kuutaka viongozi wao
waachane na hoja zingine zote na kuijadili hiyo
ya hisa.
Kikao hicho ambacho kiliendeshwa chini ya ulinzi
mkali wa Polisi kilianza saa 2 asubuhi, ambapo
wanachama wengi walifika wakiwa na ajenda ya
kutaka kuuzwa kwa hisa na si vinginevyo.
Kwa sasa Simba inaonekana kusuasua katika
vyanzo vyake vya mapato baada ya kujitoa kwa
mdhamini, Kampuni ya Bia ya Kilimanjaro
ambayo ilikuwa ikizidhamini Simba na Yanga na
kwa sasa imesitisha udhamini wake kote.
Hali hiyo imesababisha msukumo mkubwa kwa
wanachama kutaka mwekezaji wa muda mrefu
katika kampuni hiyo, ambapo hoja hiyo ilitawala
katika mkutano huo, hali iliyositisha kujadiliwa
kwa hoja nyingine.
Ilielezwa na mwanachama mmoja katika mkutano
huo kuwa kati ya hoja sita za msingi, ambazo
ziliahidiwa na Rais Evans Aveva na kamati yake
kabla ya kuingia madarakani ni moja tu ya
ulipwaji wa mishahara ndio ambayo imefanikiwa.
Alihoji ni kwa nini Aveva na kamati yake
wasijiuzulu uongozi, hali hiyo ilifanya wanachama
kushangilia na kutaka mabadiliko hayo kufanyika,
lakini hata hivyo Aveva alijikuta katika wakati
mgumu alipotaka kuzuia hoja hiyo.
Baada ya mvutano wa dakika 15 wanachama
walikubali kumsikiliza Aveva aliyetaka kujadiliwa
kwa hoja nyingine muhimu kwanza, na ndipo
akaruhusu kusikilizwa kwa ripoti ya mkaguzi wa
mapato ya Simba.
Ripoti hiyo iliendelea kubainisha madudu katika
matumizi ya fedha na kisha msomaji wake
akashauri kuwa klabu hiyo inatakiwa kuwa na
mapato ya kudumu na kushauri ujio wa
mwekezaji, hapo ndipo wanachama walipoanza
tena vurugu.
Safari hii wanachama walikataa kukaa kimya na
kuendelea kushangilia wakitaja jina la Mo kila
mahali wakiwa wanamaanisha Mohamed Dewji
apewe hisa. Hali hiyo ilidumu kwa takribani
dakika 20 kabla ya Aveva kukubali hoja hiyo ya
uuzwaji wa hisa kuingizwa kuwa ni moja kati ya
hoja za kujadiliwa na wanachama na kumaliza
kikao.
Baada ya kuvunjika kwa kikao hicho Aveva
alitolewa akiwa chini ya ulinzi mkali na kisha
kupumzishwa ndani ya bwalo kabla ya kuondoka
baada ya dakika 30.
Watu mbalimbali walitoa maoni yao kuhusu suala
hilo, ambapo mwanachama mkongwe wa klabu
hiyo Mzee Kilimoni alisema kuwa uuzwaji wa
hisa sio shida ila inaonekana ni kama kuna nguvu
imetumika kuwalaghai wanachama na kujikuta
wakishabikia bila ya kuwa na hoja ya msingi.
Kwa upande wake mwanachama na aliyewahi
kuwa kiongozi wa zamani wa Simba, Majaliwa
Mbasa, Diwani wa kata ya Sumve mkoani
Mwanza, alimlaumu Aveva kuwa ni kiongozi asiye
na uwezo wa kutoa uamuzi.
Alisema kwa sasa Aveva hana mwelekeo,
ameshindwa hata kuongoza kikao hicho na
kumalizika kihuni huku akisisitiza kuwa Simba
inahitaji mabadiliko ya kweli.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top