Breaking News
Loading...

Advert

Monday, August 1, 2016

Tundu Lissu amesema operasheni UKUTA uko palepale septemba mosi mwaka huu.soma zaid.

MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu
Lissu amesema licha ya viongozi wa chama
hicho kutishwa, kukamatwa na kuhojiwa na
Jeshi la Polisi, bado msimamo wao kuhusu
operesheni Ukuta itakayofanyika Septemba Mosi
mwaka huu uko pale pale.
Chama hicho kinatarajiwa kufanya operesheni
mpya iliyopewa jina la Umoja wa Kupambana na
Udikteta Tanzania (Ukuta).
Operesheni hiyo inatarajiwa kuwa itakwenda
sambamba na uzinduzi wa mikutano ya hadhara
nchi nzima, ambayo itafanyika Septemba Mosi,
mwaka huu.
Hatua hiyo imefikiwa na kikao cha Kamati Kuu
ya chama hicho iliyoketi kwa siku nne mfululizo
wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na kutoa
maazimio matatu ambayo yatatekelezwa na
chama hicho.
Pamoja na mambo mengine, chama hicho
kimesema lengo la operesheni hiyo ni kuzuia
matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia
nchini, kiliyodai kuwa yanafanywa na Rais Dk.
John Magufuli.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini
Dar es Salaam baada ya kuhojiwa na kuachiwa
kwa dhamana Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe, Mwanasheria Lissu alisema
msimamo wao uko palepale na hakuna
kilichobadilika.
“Wamemuhoji kwa taarifa aliyoitoa mbele ya
waandishi wa habari juu ya msimamo wa
chama wa kufanya mkutano nchi nzima. Tatizo
jeshi letu wakisikia maandamano, mkutano au
mtu anamsema Magufuli basi anatuhumiwa kwa
uchochezi, wametumia muda mrefu kumuhoji
lakini mwisho wamemwachia kwa dhamana na
amewahi ‘Airport’ ili aende kuhudhuria mazishi
ya kamanda wetu Senga (Joseph) na
watamwita watakapomwihitaji tena,” alisema
Lissu.
Alisema pamoja na hayo bado msimamo wa
chama hicho kufanya mikutano waliyoiita
Operesheni Ukuta ipo pale pale ifikapo
Septemba Mosi, mwaka huu.
“Nafikiri ni muhimu sana huko tunapoenda
kuzungumza na wenzetu hii kitu inaitwa
uchochezi ni nini? Tunashitakiwa kwa sheria ya
magazeti ya mwaka 1976 ambayo waliingiza
vifungu vya uchochezi mwaka 1978 lengo lao
kuu ni kuwafunga watu midomo na ilitungwa
wakati wa mfumo wa chama kimoja.
“Hata hivyo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere ndiye wa kwanza kushtakiwa
kwa uchochezi pamoja na mwandishi Robert
Makenge na mwenzao Rashid Bagedae, kwa
msingi huo sisi tunafuata nyayo zake,” alisema.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida
Mashariki (Chadema), alisema kuitwa
mchochezi, ni jambo la ufahari kupinga udikteta
kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere.
“Nasema hivyo kwa sababu Mwalimu Nyerere
ndiye wa kwanza kuitwa mchochezi, ni kitendo
cha kufunga watu midomo ili washindwe
kuwaita watu wajinga pale wanapofanya ujinga.
“Tume ya Jaji Nyalali mwaka 1992 wakati
mfumo wa vyama vingi unatambulishwa na
kuanza nchini ilipendekezwa sheria hii ifutwe
kwa sababu haiendani na mfumo uliopo lakini
hakuna kilichofanyika,” alisema.
Mwanasheria huyo ambaye naye amefunguliwa
kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Kisutu
jijini hapa, aliwataka wafuasi wa chama hicho
kujitokeza kwa wingi Agosti 2, mwaka huu
mahakamani hapo.
“Dawa yao si majaji bali umma… umma ufurike,
tutawashinda hawa watu makesi yenyewe ni
haya ambayo hayana kichwa wala miguu,”
alisema na kushangiliwa na wafuasi wa chama
hicho.
Mbowe alifika kituoni hapo akiwa ameongozana
na viongozi mbalimbali wa Chadema akiwamo
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ambaye
hata hivyo alizuiwa kuingia katika chumba cha
mahojiano.
Askari waliokuwa kwa wingi katika eneo hilo,
walisikika wakisema kuwa anayepaswa kuingia
ndani ni Mbowe, Mwanasheria Tundu Lissu na
Wakili wa Chadema, John Mallya.
Lowassa, wafuasi wa Chadema na waandishi
wa habari walilazimika kubaki nje huku askari
wakiimarisha ulinzi wakiwa wamebeba bunduki
zao huku magari yenye maji ya kuwasha yakiwa
yameegeshwa pembeni.
Wakati chama hicho kikijiandaa kutekeleza
Operesheni Ukuta Septemba Mosi, tayari Rais
Magufuli amezuia operesheni hiyo na kuwaonya
wale wote watakaokaidi agizo lake na kuamua
kuandamana.chnzo muungwana blog

0 comments :

Post a Comment

Back To Top