Breaking News
Loading...

Advert

Monday, August 1, 2016

Wakurugenzi watakao toa taarifa za uogo watafutwa kazi.soma zaid.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
Serikali haitasita kuwaondoa katika nyadhifa zao
Wakurugenzi wote watakaoshiriki katika kutoa
taarifa za uongo kuhusu miradi mbalimbali ya
maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
“Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kutekeleza
miradi ya maendeleo ambapo kuna baadhi ya
viongozi wamekuwa wakiandika taarifa za uongo
kuwa mradi umekamilika wakati haujajengwa,
hivyo wakurugenzi watakaoshiriki kutoa taarifa
zisizokuwa sahihi wataondolewa,” alisema.
Waziri Mkuu ameyasema hayo jana jioni
(Jumapili, Julai 31, 2016) wakati akipokea
taarifa ya mkoa wa Morogoro mara baada ya
kuwasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya
siku tatu.
Alisema alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa
wakurugenzi katika halmashauri zote nchini
kuhakikisha wanatembelea miradi yote
inayojengwa katika maeneo yao ili kufanya
ukaguzi na kujiridhisha kama thamani yake
inalingana na kiasi cha fedha kilichotolewa.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema
Serikali aihitaji Halmashauri kutoa ajira za
mikataba kwenye kada zilizopo katika muundo
wa ajira hivyo ameziagiza halmashauri zote
nchini kufanya mapitio ya watumishi wa
mikataba.
“Tumeruhusu kuajiri kwa mikataba walimu wa
masomo ya sayansi kwa kipindi cha miaka miwili
tena kwa waliostaafu. Kuna kada zilizoko katika
muundo wa ajira hizo hatuhitaji watumishi wa
mikataba wakiwemo madereva msiwatumikishe
kwa mikataba watakosa stahili zao,” alisema.
Akizungumzia suala la watumishi hewa mkoani
Morogoro Waziri Mkuu alisema ni vema
wakaendelea kufanya uchunguzi na ifikapo
mwisho wa mwezi huu wawe wamekamilisha
taarifa na kuanza kuchukua hatua kwa
waliohusika kwa waliohusika.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro
Dk. Stephen Kebwe katika taarifa yake
aliyoiwasilisha kwa Waziri Mkuu alisema mkoa
unaendelea kutekeleza agizo la Rais Dk. John
Magufuli la kuzitaka taasisi zote za Serikali
kufanya uhakiki wa mishahara hewa na malipo
batili ya watumishi.
Alisema mkoa umebaini watumishi hewa 315
ambao wameisababishia Serikali hasara ya sh.
bilioni 2.132 ambapo timu ya uhakiki bado
inaendelea na zoezi hilo na taarifa kamili
itatolewa mara kazi hiyo itakapo kamilika.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top