Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, August 11, 2016

Ngariba Aliyekeketa Watoto wa kike zaid ya 5,000 kwa miaka 13 Aokoka.som zaid

Ngariba Aliyekeketa Watoto wa Kike Zaidi ya
5,000 kwa Miaka 13 Aokoka
 Habari, Kitaifa  August 11th, 2016
 0 Comments
Serengeti, Mara
Ngariba Nguli wa ukoo wa Wanyabasi ambaye
amekeketa watoto wa kike zaidi 5, 000 kwa
kipindi cha miaka 13 iliyopita amedai
ameachana na kazi hiyo baada ya ‘kuokoka’.
Ngariba huyo, Mkazi wa Kijiji Rung’abure,
Christina Mairo (55) maarufu kwa jina la Wansato
alifikia uamuzi huo baada ya kuhubiriwa na
wachungaji wa Kanisa la Jeshi la Wokovu
waliomtembelea nyumbani kwake kumweleza
madhara ya kukeketa watoto wa kike.
Pamoja na ‘kuokoka’ na kutangaza kuachana na
shughuli hiyo, ngariba huyo pia aliteketeza mkoba
wake wenye zana za ukeketaji baada ya
kuingiwa na somo la ubaya na madhara ya
ukeketaji.
Akizungumza baada ya kutangaza kuacha kazi
hiyo na kuchoma moto zana za ukeketaji,
Ngariba huyo alikiri kushuhudia mateso
wanayopata wanawake walikeketwa wakati wa
kujifungua watoto.
Mairo amesema ameamua kuachana na kazi hiyo
ambayo inamfanya kuandamwa baada ya kujua
matatizo yanayowakumba wajawazito wakati wa
kujifungua.
Mratibu wa mradi wa kutokomeza vitendo vya
ukatili wa kijinsia Kupitia Jumuiya ya Kikristo
Tanzanja (CCT), Sophia Mchonvu alisema kwa
kipindi cha miaka 10, shirika hilo na wanaharakati
wamekuwa wakimtembelea ngariba huyo
kumshawishi kuachana na kazi hiyo bila
mafanikio.
“Tukio la ni matunda ya harakati zilizoanza miaka
10 iliyopita. Hii ni ishara njema katika
mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa
kijinsia wilayani Serengeti na maeneo mengine
ambako vitendo vya ukeketaji vinafanyika,”
alisema Mchonvu .
Mchungaji wa kanisa hilo, Wilson Mwile alisema
vita dhidi ya ukatili vinakwamishwa na imani, mila
na desturi kandamizi dhidi ya wanawake.
Diwani wa Kata ya Rung’abure, Elias Mirengo
aliwataka ngariba wengine kuacha shughuli hiyo.
Mmoja wa watoto wa ngariba huyo, Rachel
Thomas aliwashukuru waliofanikisha mama yake
kuachana na kazi hiyo ya ukeketaji watoto wa
kike.
CHANZO: Mwananchi

0 comments :

Post a Comment

Back To Top