Walimu mkao wa Dar es salaam kusafiri bure kwenye treni.soma zaid
Dar es Salaam,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda amewatangazia walimu wa mkoa huo,
kuanza kusafiri bure kwenye treni baada ya
kuingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania
(TRL).
Hatua hiyo imekuja ikiwa miezi michache imepita
tangu, kiongozi huyo kuanzisha mfumo wa
walimu kusafiri bure kwenye daladala wakati
akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makonda
alisema walimu watasaifiri bure katika njia za
Stesheni-Ubungo Maziwa na Stesheni –Pugu
ambako treni zinafanya safari zake.
“Kinachotakiwa ni kuwa na vitambulisho kutoka
kwa wakuu wa shule, wakionyesha hakuna
atakayewahoji hivyo watasafiri bure,”alisema
Makonda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania,
Masanja Kadogosa alisema walimu
watasafirishwa kwa nidhamu kubwa.
0 comments :
Post a Comment