Reginal Mengi ameiomba mahakama ajitete ili asifungwe.soma zaid
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kampuni za IPP,
Reginald Mengi ameiomba Mahakama Kuu
Kitengo cha Biashara kuwasilisha utetezi kwa
njia ya kiapo ya kwa nini asifungwe jela kwa
kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama
hiyo katika kesi ya ununuzi wa hisa.
Mengi alitoa maombi hayo jana kupitia kwa
wakili wake, Deogratius Ringia baada ya amri ya
Mahakama hiyo iliyotolewa na Jaji Mfawidhi,
Amir Mrumi, Agosti 9, mwaka huu, ikimtaka
afike mahakamani hapo jana kujieleza kwa nini
asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu
hiyo.
Mahakama hiyo katika hukumu yake iliyotolewa
na Jaji Aghaton Nchini na kusomwa katika kesi
ya msingi ya madai iliyofunguliwa na
wafanyabiashara watatu, ilimwamuru Mengi
kuwalipa jumla ya Sh1.2 bilioni.
Licha ya Wakili Ringia kukanusha kwenye
vyombo vya habari kuwa Mengi hahusiki katika
kesi hiyo aliyotakiwa kufika mahakamani
kujitetea kwa nini asifungwe, jana wakili wake
huyo alifika mahakamani hapo na kudai mteja
wake ameshindwa kufika kwa sababu anaumwa.
Pamoja na kuiarifu Mahakama kuwa Mengi
ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa
anaumwa na yuko kwenye mapumziko, aliiomba
Mahakama impe siku 14 ili aweze kuwasilisha
kiapo chake cha utetezi, madai ambayo
yalipingwa na wakili wa wadai, Mafuru Mafuru.
0 comments :
Post a Comment