Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, August 25, 2016

Ronaldo mwanasoka bora barani Ulaya 2015/2016.soma zaid


Nyota wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno
Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya mwanasoka
bora wa Ulaya kwa msimu wa 2015/15 katika
sherehe zilizofanyika leo, mjini Monaco nchini
Ufaransa.
Cristiano Ronaldo akiwa na tuzo yake
Ronaldo ametwaa tuzo hiyo akiwabwaga
wenzake Gareth Bale wa Real Madrid pia na
Antoine Griezmann w Atletico Madrid waliofikia
hatua ya tatu bora.
Kwa mujibu wa kura 55 zilizopigwa, Ronaldo
amepata kura 40, akifuatiwa na mfaransa
Antoine Griezmann aliyepata kura 8, huku Gareth
Bale raia wa Wales akiambulia kura 7 pekee.
Zoezi la upigaji kura liliwashirikisha waandishi 55
wa habari za michezo kutoka nchi wanachama
wa UEFA.
Baadhi ya mambo yalichongia Ronaldo kupata
tuzo hii ni pamoja na ubingwa wa michuano ya
Ulaya kwa ngazi ya vilabu ambapo aliiongoza
Real Madrid kutwaa kombe la Mabingwa Ulaya
(UEFA Champions League) kwa msimu huo,
kabla ya kuiongoza timu yake ya Taifa ya Ureno
kutwaa kombe la Mataifa ya Ulaya UEFA EURO
2016.
Katika msimu huo, Ronaldo amecheza mechi 36
za ligi ya Hispania (La Liga), na kufunga magoli
35 huku akisaidia (assist) magoli 11.
Katika michuano ya Mabingwa Ulaya amecheza
mechi 12, akifunga magoli 16 na kusaidia magoli
4.
Katika michuano ya Mataifa Ulaya (UEFA EURO
2016) amecheza mechi 7 na kufunga magoli
matatu huku akisaidia magoli matatu.
Hii ni mara ya pili kwa Ronaldo mwenye umri wa
miaka 31 kutwaa tuzo hiyo baada ya kufanya
hivyo katika msimu wa 2013/14.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top