LHRC.vyama vya siasa vishindane kwa hoja na viache kutumia vyombo vya dola.soma zaid
LHRC yaitaka serikali kuheshimu haki za
binadamu
THURSDAY , 25TH AUG , 2016
Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini
LHRC kimeishauri serikali kulinda na kuheshimu
haki za binadamu kama zilivyoainishwa kwenye
Katiba ya Tanzania na sheria za nchi kama
walivyoapa kuzilinda kwenye kiapo chao cha utii
na uongozi.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dkt. Hellen
Kijo-Bisimba
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dkt. Hellen Kijo-
Bisimba wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya
habari kuhusu hali ya haki za kiraia na kisiasa
zilivyo kwa sasa nchini.
Dkt. Kijo-Bisimba amesema vyombo vya dola na
viongozi wa serikali hususani Jeshi la Polisi
kufanya kazi kwa weledi, kufuata sheria na
taratibu zake bila kuwatisha na kuwajengea hofu
wananchi.
Amesema vyama vya siasa nchini vishindane kwa
hoja na kuacha kutumia vyombo vya dola katika
kushinikiza hoja au matakwa yao, na kwamba hali
hiyo itasaidia kukuza na kuimarisha haki za
binadamu na democrasia nchini na kuleta usawa
na ushindi wa kweli.
Amesema kushindana kwa hoja pia ni fursa kwa
wananchi na watanzania kusikia, kuelewa na
kupambanua hoja na kujenga jamii yenye uelewa
na upeo mpana kuhusu masuala yanayowahusu
ya ndani na nje ya nchi.
Amesema Msajili wa vyama vya siasa asimamie
katika nafasi yake ya mratibu, msimamizi na
mbeba bendera ya maendeleo ya vyama vya
siasa na ukuaji wa democrasia na kutojiingiza
katika kuonekana kuegemea upande au chama
chochote ili kusaidia kujenga mshikamano wa
taifa na uimarishaji wa democrasia na vyama vya
siasa.
Kwa upande wa tume wa haki za binadamu na
utawala bora Dkt Bisimba ameishauri iendelee
kusimamia haki za binadamu na kuishauri serikali
na mamlaka zake kila mara kuhusu heshima na
ulinzi wa haki za binadamu nchini.
Pia ametaka mchakato wa upatikanaji wa katiba
mpya urudishwe na kuendelezwa ili kupata katiba
bora itakayoanzisha vyombo huru na mifano
imara ya uwajibikaji ili kusaidia ulinzi wa haki za
binadamu, demokrasia na uwepo wa maendeleo
endelevu.chanzo eatv.
0 comments :
Post a Comment