Afsa Ardhi na mipango miji atumbuliwa Bunda mkoan mara.sima zaid.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri
ya mji wa Bunda mkoani Mara, Bibi.
Janeth Mayanja amemsimamisha kazi
mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango
Miji kwa kosa la kujipatia fedha kinyume
na taratibu za utumishi wa umma.
Akizungumza leo mjini Bunda wakati wa
tukio hilo, Bibi. Mayanja alisema kuwa
ameamua kumsimamisha kazi kwa muda,
Bw.Eliudi Haonga ambaye ni mtumishi wa
Idara ya Ardhi na Mipango Miji pia ni
Mthamini wa Halmashauri hiyo ili
kupisha uchunguzi kwa kosa la kujipatia
fedha kinyume na taratibu za utumishi wa
umma.
“Tarehe 28 mwezi Juni mwaka huu
Bw.Eliudi Haonga alipokea fedha kiasi
cha shilingi milioni saba kutoka kiwanda
cha Olam ikiwa ni kodi ya pango kwa
mwaka kodi 2015/2016, lakini mtumishi
huyo alihifadhi kwenye akaunti ya
Halmashauri ya mji yaani ‘own source’
fedha kiasi cha shilingi milioni mbili tu,
na kiasi kilichobaki yaani milioni tano
alizitumia kwa masuala binafsi kinyume
na taratibu za utumishi wa umma”
alisema Bibi Mayanja
Aliongeza kuwa Bw. Haonga aligushi risiti
ya Halmashauri ya Mji na ambayo
aliikabidhi katika kiwanda cha Olam
baada ya kupokea fedha hizo.
Alisisitiza kuwa mtumishi huyo
amesimamishwa kazi kwa mujibu wa
kifungu namba 38 (1) cha kanuni za
utumishi wa umma za mwaka 2003.
Aidha, Bibi Mayanja amewaasa
watumishi wa umma wanaofanyakazi
katika Halmashauri hiyo kuwa waadilifu
kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za
nchi. Vile vile ameonya kuwa hatua kali
za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote
atakayekiuka.
0 comments :
Post a Comment