Rais Mugabe ameagiza kukamatwa wanamichezo wote waliokwenda kwenue mashindano ya Olympic Brazil 2016.soma zaid
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemwagiza
mkuu wa Polisi wan chi hiyo Augustine Chihuri
kuwakamata wachezaji wote wa timu iliyokwenda
inchini Brazil kwenye mashindano ya Olympic
mara tu watakapokanyaga kwenye ardhi ya
uwanja wa ndege wa Harare.
Zimbabwe ni miongoni mwa mataifa ambayo
wanamichezo wake hawakufanikiwa kushinda
medali ikiwa inawakilishwa na wanamichezo 31.
Mchezaji ambaye alionekana kufanya vizuri ni
yule aliyekamata nafasi ya nane
Mugabe amemwambia mkuu huyo wa polisi
kuwakamata wanamichezo hao: Tumepoteza
pesa za taifa kwa ajili ya hao panya tunaowaita
wanamichezo. Kama hauko tayari kujitoa na
kushinda japo medali ya shaba kama wenzetu wa
Botswana walivyofanya, sasa kwanini ulienda
kupoteza pesa zetu” alisema.
Kama tulihitaji watu kwenda Brazil kuimba wimbo
wetu wa taifa na kupeperusha bendera,
tungewaagiza warembo na vijana watanashati
kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe
wakatuwakilishe.
Akaongeza kwamba, pesa iliyowekezwa kwenye
timu ili kuiwakilisha inchi ingeweza kutumiwa
kununulia dawa na kujenga shule. Jambo hili ni
sawa na mwanaume asiyelijali kuoa wanawake
watano, maana yake nini? Nitahakikisha
tunagawana hasara, wote watailipa serikali bila
kujali hata kama itachukua miaka 10, sasa pesa
hizo zinabadilika na kuwa mkopo tuliowapa
kwenda Brazil kama watalii, hawana faida”
akamaliza.
0 comments :
Post a Comment