Breaking News
Loading...

Advert

Friday, August 12, 2016

Tanzania yaitaka uturuki itoe ushahidi.soma zaid

Serikali ya Tanzania yasema haina
ushahidi wa kutosha kuzitia hatiani shule
za Feza zinazodaiwa kumilikiwa na raia wa
Uturuki anayetuhumiwa kujihusisha na
jaribio la kupindua Serikali ya Uturuki.
Serikali ya Uturuki inadai wamiliki wa
shule hizo na baadhi ya wafanyabiashara
wanafadhili ugaidi kwa kushirikiana na
Imamu Fethullah Gulen anayeishi nchini
Marekani ambaye ndio inadaiwa yuko
nyuma ya jaribio la Mapinduzi.
= > Serikali ya Uturuki yatakiwa
kuwasilisha taarifa zenye ushahidi wa
kutosha juu ya hili.
= > Aidha, Ubalozi wa Uturuki Tanzania
umedai kuwa baadhi ya walimu wa shule
za FEZA ambao ni raia wa Uturuki
wamekuwa wakitumia mbinu za kigaidi
kufundisha wanafunzi.
=======
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano
wa kimataifa Augustino Mahiga
amesema serikali ya Uturuki kupitia
balozi wake hapa nchini imedai
wamiliki wa shule za Feza Tanzania
walifadhili jaribio la mapinduzi Uturuki
Serikali hiyo inadai mapinduzi hayo
hayakuanzia jeshini tu bali yameanzia
kwenye vyuo na shule mbalimbali
Uturuki na nje ya uturuki
Ubalozi wa Uturuki umesema wamiliki
wa shule hizo hapa nchini wanahusika
na kufadhili mapinduzi hayo huko
Uturuki na ada inayokusanywa kutoka
kwenye shule hizo ilitumika kufadhili
mapinduzi hayo na ni magaidi
Balozi Mahiga amesema wametaka
ushahidi zaidi kutoka serikali ya
Uturuki kuhusu madai hayo
Walimu wa shule ya Feza wamedai
wao hawahusiki kabisa na mapinduzi
hayo na shule zao hazijihusishi na
mambo ya siasa na zinamilikiwa na
watanzania.chanzo jamii forums.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top