Ufisad sh.190 zilizo tolewa kwa ajili ya fidia zinadaiwa kutafunwa na baadhi ya watendaji mkoani mbeya.soma zaid
ZAIDI ya Sh milioni 190 zilizotolewa na Serikali
kwa ajili ya ulipaji wa fidia wananchi wa vijiji 21
wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya, zinadaiwa
kutafunwa na baadhi ya watendaji wa
halmashauri hiyo.
Fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya kulipa fidia
wananchi hao ili wahame kupisha Hifadhi ya
Taifa ya Ruaha, ambazo zilitakiwa kulipwa
pamoja na kujenga shule ya msingi na zahanati
ya ya Kijiji cha Ikoga Mpya.
Kutokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), alibaini
fedha hizo kupotea huku wananchi wa vijiji 21
wakiwa hawajalipwa fidia hiyo.
Hali hiyo ilimfanya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Amos Makalla, akuingilia kati na kuhoji
waliohusikana na ubadhirifu huo.
“Ulipwaji wa fedha hizi ulighubikwa na
udanganyifu mkubwa, taarifa ya CAG imetoka
katika ulipaji wa fidia kiasi cha shilingi milioni
192 zimeliwa na wajanja,”alisem Makalla
alipokuwa akizungumza na wanakijiji wa Ikoga
Mpya.
Alisema CAG amebaini kuwapo kwa baadhi ya
watu ambao hawakufanyiwa tathmini lakini
walilipwa fedha huku taasisi kama shule,
zahanati na msikiti fedha zao zikitafunwa na
wajanja wachahe.
“Mtu hayupo eneo la tukio lakini kaandikwa jina
kachukua shilingi milioni 26, anaitwa Twaha
Mlidi Jemedali anatoka Kijiji cha Upagama
Kitongoji cha Mbuyuni, yeye ana duka la dawa.
“Alikuwa mfanyabiashara akajiingiza na kulipwa,
pili shilingi milioni 156 zilitolewa kwa ajili ya
kujenga shule, zahanati lakini zimeliwa lakini
kubwa zaidi ni pale watu wamediliki hata kula
fedha za ujenzi wa Msikiti wa Msangaji shilingi
milioni 9,” alisema.
Kutokana na hali hiyo Makalla, alisema kuwa
watendaji waliohusika ni lazima wasakwe na
wachukuliwe hatuaza kisheria licha ya
kuhamishiwa kwenye maeneo mengine.
“Lazima hawa wachukuliwe hatua kali za
kisheria pamoja na kuzirejesha fedha hizi, hata
kama mtu huyo atakuwa Manyara au Musoma
aitwe ili haje kujibu mashtaka haya,” alisema
Makalla.
0 comments :
Post a Comment