Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, August 18, 2016

TRA imesema matengenezo ya EFD's yatakuwa bure.soma zaid


Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imesema
kuwa hakuna mfanyabiashara anayepaswa
kutozwa pesa kama malipo ya matengenezo ya
mashine ya kutoka risti ya EFD pale
itakapohitaji matengenezo.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Kwa Mlipa
Kodi kutoka TRA bwana Richard Kayombo
amesema kumekuwa na malalamiko kutoka
wafanyabiashara kuwa wamekuwa wakitozwa
pesa ya matengenezo na wasambazaji wa
mashine hizo jambo linalowakatisha tamaa
kuendelea kutumia machine hizo.
Hata hivyo Kayombo amesema kuwa kama
matengenezo yatahusiana na uharibifu
uliotokana na uzembe wa mtumiaji, atalazimika
kulipia gharama za matengenezo.
"Kama imeharibika kwa uzembe wako mfano
umeiangusha nchini, au imetumbukia kwenye
maji, ni lazima ulipie, kwahiyo ni jukumu lako
kuwa lakini, lakini kama ni matatizo yanayohufu
mfumo wenyewe au msambazi, basi hakuna
mtu atakayelipishwa" Amesema Kayombo
Kuhusu malalamiko ya mashine kutokuwa na
mtandao (network), Kayombo amesema licha ya
kwamba mashine hizo huwa zimeuganishwa
katika mtandao maalum, zoezi la kutoa risiti
halihitaji mtandao, hivyo amesema pasiwe na
kisingizio kama hicho kama njia ya kukwepa
kutoa risiti.
Kayombo pia amepongeza jitihada zinazofanywa
na Rais Magufuli za kuhamasisha watanzania
kulipa kodi kwa hiari, kuwa sasa mwamko wa
watu umekuwa mkubwa, na mwitikio ni mzuri
kwa kuwa watu wanaona matumizi ya kodi yao.
Ameendelea kutoa onyo kwa baadhi ya
wafanyabiashara wasiotumia mashine za EFD,
lakini pia wateja wasiokuwa na tabia ya kudai
risiti, akiwataka kubadilika mapema kwa hiari
yao kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa
dhidi yao.
"Kuna watu bado hawapendi kudai risiti, hata
wakipewa hawataki, mfano kwenye vituo vya
mafuta vilivyo vingi, kuna mashine za EFD, mtu
akinunua mafuta akipewa risiti anaikataa au
kuiacha hapohapo kituoni, jambo ambalo
limelalamikiwa na wauzaji kwa kusababisha
uchafu," Amesema Kayombo.
Amesema watu wa aina hiyo wakikamatwa,
wakikamatwa, hatua ya kwanza ni kupewa onyo,
hatua ya pili ni kufikishwa mahakamani na
hatua ya tatu ni kufungiwa biashara kwa
upande wa wafanya bishara.
Mashine za EFD

0 comments :

Post a Comment

Back To Top