February 19, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, August 4, 2016

Wakurugenzi wawili wa shirika la ndege Tanzania (ATCL) wamesimamishwa kazi.soma zaid.

Wamesimamishwa kwa kupeleka
marubani wasiokidhi vigezo kwenye
mafunzo nje ya nchi.
Zoezi endelevu la kusimamisha kazi
kupisha uchunguzi limeendelea ambapo
leo asubuhi viongozi wawili wa ATCL
wamesimamishwa kazi.
Mmoja wa viongozi hao ni aliyekuwa CEO
wa ATCL ENG JOHNSON MFINANGA.
Waziri ameapa kupambana na wale wote
watakaofanya kazi kwa mazoea.
==========
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa ATCL
asimamishwa kazi kwa kosa la
kumchagua rubani asiye na sifa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasilianoa prof.MAKAME MBARAWA
amemsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi
mkuu wa shirika la ndege Tanzania ATCL
Captain Jonson Mfinanga na Mkurugenzi
wa uendeshaji Captain Sadick Muze kwa
kosa la kuchagua rubani mmoja asiye na
sifa kati ya marubani watano wanaotarajia
kuondoka hapo kesho kwenda nchini
Canada kwa ajili ya mafunzo ya kurusha
ndege mpya zinazotarajiwa kuwasili
nchini katikati ya mwezi Septemba.
Akizungumza na waandishi wa habari
mkoni Mbeya Pro.Mbarawa amesema
baada ya kukamilisha malipo ya awali ya
ununuzi wa ndege mbili mpya kwa ajili ya
shirika la ndege Tanzania ATCL alitoa
maelekezo kwa kaimu Mkurugenzi Mkuu
huyo kuwachagua marubani watano
wenye sifa ili waende nchini Canada kwa
ajili ya mafunzo ya kurusha ndege hizo
pindi zitakapo wasili jambo ambalo
amesema miongoni mwa marubani hao
watano waliochaguliwa mmoja hajatimiza
vigezo hivyo kuamua kumsimamisha kazi
kwa kosa la uzembe.
Aidha waziri huyo amesisitiza kuwa
msimamo wa serikali ni kuhahakikisha
kila mtumishi wa umma anatekeleza
wajibu wake kwa kufuata sheria kanuni
na taratibu hivyo atakaye kiuka msimamo
huo haitasita kumchukulia hatua kali
zakinidhamu.
Chanzo: ITV

0 comments :

Post a Comment

Back To Top