Breaking News
Loading...

Advert

Friday, August 5, 2016

Raia ,2 wa kigeni wakatwa kwa kuwa watumishi wa serikali.soma zaid

RAIA wawili wa Kigeni wakamatwa jijini
Dar es Salaam kwa kosa la kuishi hapa
nchini bila kibali na kuwa watumishi wa
Serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Idara ya
Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John
Msumule amesema kuwa Raia hao
ni Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa
jina la Roy Bilingita raia wa Congo
na Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba
raia wa Malawi.
Amesema kuwa Bw.Bahilanya Milingita
maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa
Congo ambaye anatuhumiwa kuingia
nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
kinyume na sheria za nchi, na Dkt. Esther
Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi
ambaye alikuwa Mganga Mkuu katika
kituo cha Afya Mburahati anatuhumiwa
kufanya kazi Serikalini wakati si raia wa
Tanzania.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar
es Salaam John Msumule akisisitiza jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa
ya kukamatwa kwa watumishi wawili wa
Serikali ambao sio raia wa Tanzania
mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa ambao sio raia wa Tanzania
waliokuwa wakifanya kazi serikalini
wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa
Uhamiaji, kushoto ni Bw. Bahilanya
Milingita aliyekuwa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO)na kulia ni Dkt.
Esther Green Simon Mwenitumba ambaye
alikuwa Mganga Mkuu Kituo cha Afya
Mburahati.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top