Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, August 4, 2016

serikali imetenga 900m kuzalisha dawa za binadamu viwanda vya ndani.soma zaid.

Serikali imetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa
za binadamu katika viwanda vya ndani ili
kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa nje
zipatikane nchini.
Akizungumza hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi
mpya ya ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na
dawa nchini (TFDA), Waziri wa Afya Waziri wa
Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali
imetenga fedha hizo kuhakikisha viwanda vya
ndani vinatengeneza dawa hapa nchini na kupiga
hatua katika uchumi wa viwanda.
“Serikali kupitia wizara yangu tumetenga milioni
900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika
viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa kati kwa
kutumia viwanda,” alisema Mhe. Ummy.
Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA kwa
kushirikiana na Serikali wanapaswa kuhakikisha
viwanda vya ndani vinatengeneza dawa zenye
ubora kwa matumizi ya binadamu ili kupunguza
magonjwa yanayotokana na sumu za kemikali
zitokananzo na dawa hizo.
Mhe. Ummy ameongeza kuwa TFDA inatakiwa
ishirikiane na Taasisi ya viwango nchini (TBS)
ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa zisizokizi
viwango na ubora unaopaswa kutumiwa na
Watanzania.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa TFDA
inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili
kuwawezesha watanzania kuepuka kutumia
bidhaa zisizo na ubora kwa matumizi ya
binadamu.
Mbali na hayo Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA
inatakiwa ikusanye mapato kwa wingi zaidi ili
kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kupiga
hatua kiuchumi ili isaidie wananchi katika
shughuli za maendeleo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
TFDA Balozi Dkt.Ben Moses amesema kuwa
wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na Mhe.
Waziri na watayafanyia kazi kwa haraka na
ufanisi ili kuendana na kasi ya “HAPA KAZI TU”.
“Tumepokea maagizo ya Mhe. Waziri na nataka
kumuhakikishia kwamba tutaendelea na kasi
yetu ili kuifikisha nchi yetu kwenye kilele cha
maendeleo na Afya bora” alisisitiza Dkt. Moses.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top