Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, August 4, 2016

Tundu Lissu amefikishwa kituo cha polisi cha kati jijini Dar kwa mahojiano.soma zaid

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki
amefikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini
Dar es Salaam kwa mahojiano, polisi wamekuwa
na kazi ya ziada, anaandika Shaban Matutu.

Idadi ya polisi kwenye kituo hicho
imeongezwa wakati alipofikishwa huku
shughuli nyingine ndani ya kituo hicho
zikionekana kusimama.
Awali, Lissu ambaye ni Mwanasheria wa
Chadema hakua akijulikana alipo kutokana na
polisi kutotoa taarifa kamili baada ya kumkamata
jana jioni.
Lissu amefikishwa kwenye kituo hicho leo saa
7:54 mchana na gari aina ya Land Cruser lenye
namba za usajili T 312 CWM akiwa chini ya ulinzi
mkali.
Amefikishwa kwenye kituo hicho kwa ajili ya
mahojiano kutokana na madai ya kutoa kauli ya
kichochezi ‘dikteta uchwara’ juzi wakati akiwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
alipoenda kusikiliza kesi ya uchochezi iliyohusu
kauli yake ya awali ya ‘dikteta uchwara’.
Wakati Lissu akifikishwa eneo la kituo hicho,
polisi walikuwa wamezunguka eneo hilo huku
kukiwa na ulinzi mkali pamoja na silaha za moto.
Askari waliokuwa eneo hilo walikuwa
wakiwaondoa wananchi na waandishi wa habari
waliokuwa wakifuatilia matukio katika eneo hilo.
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa
alifika kituoni hapo saa kumi kasoro, hata hivyo
alizuiwa kuingia ndani.
Saa 4:02 Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es
Salaam kituoni hapo na gari lenye namba za
usajili SM 10584 ambapo aliruhusiwa kuingia
ndani kumuona Lissu ambaye anahojiwa.
Lissu bado anaendelea hojiwa…
 12

1

0 comments :

Post a Comment

Back To Top