Walimu watatu wasimamishwa kazi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi mkoan kagera.soma zaid.
Karagwe. Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoani
Kagera, Godfrey Mheluka amewasimamisha kazi
walimu watatu wa Shule ya Sekondari Kituntu
kwa madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na wanafunzi shuleni hapo.
Pia, ameunda kamati kuchunguza tukio hilo
ambayo ameipa siku 14 ikamilishe kazi hiyo.
Akitoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule
hiyo, Mheluka alisema zipo taarifa nyingi
zinazoripotiwa kwenye ofisi yake kuhusiana na
vitendo hivyo.
Alisema ili kudhibiti hali hiyo, ameamua
kuwasimamisha kazi walimu hao kupisha
uchunguzi.
“Hatuwezi kukubali kuona mwanafunzi
anageuzwa mke wakati mzazi kajinyima na
kumhudumia mwanaye ili asome kwa ajili ya
manufaa yake ya baadaye, na ikibainika kweli
wanafanya vitendo hivyo, hatua za kisheria dhidi
yao zitachukuliwa,” alisema Mheluka.
Hata hivyo, miongoni mwa walimu waliotajwa,
Deodatus Lusatu alikanusha kuhusika na
vitendo hivyo huku akidai kuwa anafanyiwa hila
na watu wenye nia mbaya na yeye.
Alimpongeza mkuu wa wilaya kwa kuunda
kamati ya uchunguzi, huku akitaka watu wote
wenye ushahidi dhidi yake, wajitokeze mbele ya
kamati hiyo ili ukweli ufahamike badala ya
kuendelea kumpaka matope.
“Siwezi kufanya matendo ya kishetani kama
haya, nina akili timami na kama ninafanya
vitendo hivyo sipaswa kuendelea kuwapo chini
ya jua,” alisema Lusatu.
Mkuu wa Wilaya Mheluka alisema utaratibu
wote wa kiutumishi utafuatwa bila kumuonea.
Katibu wa Tume ya Nidhamu na Maadili ya
Walimu (TSD) Wilaya ya Karagwe, Fredrick
Kabendwe alisema, atafanya kazi sanjari na
kamati atakayoiunda ili kubaini ukweli wa
tuhuma hizo.
Mkazi mmoja wa wilaya hiyo, Sadiki Juma
alisema tuhuma hizo zinapaswa kuchunguzwa
kwa makini kwani zinaweza kuwa ni chuki
binafsi.
Katika hatua nyingine, Mheluka aliwataka
wazazi, walezi na wananchi wa wilayani
Karagwe kutoa ushirikiano kwa Serikali ili
kuiwezesha sekta ya elimu kufikia malengo
wanayokusudia.
Pia, aliwataka kutunza na kuhifadhi mazingira
kwa kupanda miti na kuacha kutochoma moto
ovyo, yeyote atakayebainika sheria itachukua
mkondo wake.chanzo muungwana blog
0 comments :
Post a Comment