Serikal kutoa Ajira Mpya 71,496.soma zaid
Serikali Kutoa Ajira Mpya 71,496 Hivi
Karibuni
Serikali inatarajia kutoa ajira mpya
zipatazo71,496 kwa mwaka huu wa fedha baada
ya kukamilika kwa zoezi la kuwaondoa
wafanyakazi hewa ambapo hadi sasa watumishi
wapatao 839, tayari wapo katika hatua
mbalimbali wakiwepoo waliopelekwa katika
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU).
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,(Utumishi na
Utawala Bora),Angela Kairuki aliyasema hayo
wakati akizungumzia juu ya utekelezaji na
mikakati katika Wizara yake katika kipindi cha
“Utekelezaji” kinacho rushwa kupitia Shirika la
Utangazaji Tanzania(TBC1).
“Mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi hewa
waliofanyiwa mahojiano na polisi na kama
upelelezi ukikamilika sheria kali zitachukuliwa
ikiwepo kufikishwa mahakani kwa mtumishi
atakaye bainika kukutwa na makosa “ Alisema
Kairuki
Alisema kuwa kuna baadhi ya Maofisa Utumishi
pamoja na Wahasibu ambao wameonekana
kuwa si waaminifu kwani baadhi yao
wameonekana kuelekeza fedha kwa ndugu zao
na miradi yao na wengine walishastaafu lakini
majina yao yameonekana bado kuendelea
kuwepo katika mfumo wa kupokea.
Kairuki aliongeza kuwa katika kipindi cha Machi
mosi mpaka kufikia Agosti 20 mwaka huu,
Watumishi hewa wapatao 16,127 walibainika
ambapo walikuwa wakisababishi hasara ya
mabilioni kwa serikali ambapo serikali kama
ingewalipa ingesababisha hasara ya zaidi ya
bilioni 16.
“Uhakiki huu ni endelevu kwani baadhi ya
Maofisa Utumishi pamoja na Wahasibu si
waaminifu hivyo tunawataka waajiri wao
kuweka mkazo katika swala hili, kwani tunajua
wahasibu wengi wamepewa madaraka lakini si
waamiifu”Alisema Kiruki.
Kairuki aliwatoa hofu baadhi ya Watanzani
ambao walikuwa wakisubiria ajira mpya kutoka
Serikali, alisema kuwa kilichokuwa kikisubiriwa
ni takwimu halisi ambazo zitasaidia kuonesha ni
watumishi wangapi wameweza kuondolewa.
“hii ni neema kwa wanafunzi waliomaliza vyuo
kwani kuna nafasi zipatazo 71,496 kwa mwaka
huu wa fedha hivyo napenda kuwahauri vijana
kuwa na subira kwa kuto kujiingiza katika
makundi yasiyo faa” Alisema kairuki.
Pia aliwataka Maofisa Utumishi kuwa hudumia
vizuri watumishi kwa kuwapa haki zao ikiwemo
kuwa pandisha madaraja kwa wakati stahili na
si vema kwa baadhi ya watu kughushi taarifa za
Utumishi wa umma na kusisitiza kuwa kufanya
hivyo ni kosa kuibwa sana.
0 comments :
Post a Comment