Watanzania watakiwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa hatua anazozifanya za maendeleo.soma zaid
MWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Prof
Samwel Mwita Wangwe amesema kuwa
uongozi wa Awamu ya Tano umefanya kazi
kubwa katika kuweka maslahi ya Taifa
mbele ikiwamo kuongezeka kwa bajeti ya
maendeleo na kupunguza matumizi ya
serikali.
Hatua hii imesaidia nchi kusonga mbele
kupitia uboreshaji wa utendaji kwa
watumishi wa umma na hivyo kujenga
imani kubwa kwa wananchi juu ya Serikali
yao.
Profesa Wangwe ametoa kauli hiyo leo
jijini Dar es salaam wakati akitoa tathmini
ya uongozi wa Awamu ya Tano.
Amesema kuwa Rais Magufuli katika
uongozi wake umesaidia kuokoa fedha
nyingi za walipa kodi ambazo zilikuwa
zikiishia mikononi mwa watu wachache na
kuzielekeza katika shughuli nyingine za
maendeleo.
Profesa Wangwe amewataka wananachi
kumuunga mkono Rais Magufuli kwenye
harakati zake za kupambana na matumizi
mabaya ya fedha za umma kwa kuwa
matokeo yake yatasaidia kuijenga Tanzania
mpya ambayo kila mwananchi atapata
fursa kunufaika na rasilimali za nchi.
“Kwa kweli Rais huyu amefanya
mabadiliko makubwa sana na kwa sasa
nchi imerudi katika hali nzuri, kwani
nchi ilikuwa imefika mahali pabaya na kwa
hiyo aliona ni budi kuhakikisha Rushwa na
Ufisadi vinakomeshwa na kwa hili
ameanza vizuri na nchi inakwenda katika
mwongozo mzuri kwani ameboresha
utendaji kazini serikalini na kubana
matumizi ambayo yamesaidia kuokoa pesa
nyingi ambayo inatumika katika maendeleo
ya nchi hii”aliongeza Profesa Wangwe.
Mbali na hayo Profesa Wangwe ameshauri
Serikali kuweka mfumo mzuri katika
ukusanyaji kodi kwa kurasimisha biashara
ili mfumo huu wa EFD utumike kirahisi na
pia kutengenezwe mazingira mazuri ya
biashara kwa kuweka mazingira rahisi ya
kuandikisha biashara kwani huchukua
muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo kasi
ya kurahisisha utendaji na
wafanyabiashara watalipa kodi kwa wingi
na uchumi utakua.
Pia Profesa Wangwe ametoa ushauri kwa
vyama vya upinzani kuacha na na
maandamano yasiyo na tija na badala
yake wakae chini na kuzungumza na
serikali ilikupata mwafaka na hivyo amani
iendelee kuchanua katika nchi hii.
0 comments :
Post a Comment