Baraza la wazee wa chadema limesema kuna njama kukifuta chama cha CHADEMA.soma zaid
Dar es Salaam. Baraza la Wazee wa Chadema
limesema kuna njama za kukifuta chama hicho
zinazopangwa kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
Pia, baraza hilo ambalo limekemea vikali njama
hizo na limedai kuwa, Jaji Mutungi anafanya
hivyo ili kutimiza matakwa ya watawala kwa
kutumia mwavuli wa Baraza la Vyama vya Siasa
Tanzania.
Katibu Mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka
amesema taarifa kuhusu njama hizo
zinathibitishwa na mtiririko wa matukio ya hivi
karibuni kupitia Kamati ya Uongozi ya Baraza la
Vyama vya Siasa.
“Taarifa zimeonyesha kuwa njama hizo zinalenga
kukihujumu Chadema kwa kuandaa mitego
haramu ya kisiasa ili yatolewe mapendekezo ya
kukifuta katika orodha ya vyama vya siasa,”
alisema Lutembeka.
Hata hivyo, Lutembeka amesema Chadema
haitegemei jambo hilo kutokea kwa sababu
inafanya shughuli zake kwa kufuata misingi ya
sheria na Katiba.
Lutembeka amesema miongoni mwa matukio
hayo ni kuahirishwa kwa baadhi ya vikao
vilivyopangwa kufanyika kati ya Jaji Mutungi na
Baraza la Vyama vya Siasa.
Miongoni mambo ambayo yamepangwa
kujadiliwa kwenye mkutano huo, ni changamoto
za mfumo wa demokrasia ya vyama vingi
hususan zuio la shughuli za vyama vya siasa.chanzo mwananch
0 comments :
Post a Comment