Breaking News
Loading...

Advert

Friday, September 2, 2016

CUF yaondolewa kupisha mkutano wa Rais Magufuli Pemba.soma zaid

Jeshi la Polisi Wilaya ya Chakechake, Pemba
limezuia kufanyika mkutano na vyombo vya
habari wa Chama Cha Wananchi (CUF) uliokuwa
umepangwa kufanyika leo wilayani humo,
kupisha ziara ya Rais John Magufuli
itakayoanza leo.
Rais Magufuli anatarajia kuanza leo ziara yake
ya kwanza visiwani humo tangu achaguliwe
kuwa Mwenyekiti wa CCM.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi
ya Ikulu, Rais Magufuli atazulu Pemba leo na
kesho atakuwa Unguja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba,
Shekhani Mohamed Shekhani amesema kuwa
zuio hilo la mkutano wa CUF ni kwa sababu
eneo wanalotarajia kutumia liko jirani na eneo la
uwanja atakaokuwa akihutubia Rais Magufuli.
Hata hivyo, Katibu wa CUF wilaya ya Chake
Chake, Saleh Nassor Juma alilalamikia maamuzi
hayo ya Jeshi la Polisi kwa madai kuwa wao
walitaka kufanya mkutano na vyombo vya habari
na sio mkutano wa hadhara. Alisema kuwa
tayari walishawaeleza Idara ya Habari Maelezo
na waliridhia.
Alisema mkutano huo na waandishi wa habari
ulilenga katika kutoa tamko lao kuunga mkono
uamuzi uliochukuliwa na Baraza Kuu la chama
hicho kumsimamisha uanachama aliyekuwa
Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba
pamoja na viongozi wengine 10.
“Niliwakatalia kwa hoja kwamba mkutano na
waandishi wa habari ni haki yetu ya kikatiba na
tulikwishawataarifu watu wa Idara ya Habari
Maelezo juu ya kikao hicho halali ambacho wao
pamoja na waandishi wa habari walithibitisha
kuwa watahudhuria,” alisema Nassor.
Idara ya Habari Maelezo ilithibitisha kuwa
walikubali kufanyika kwa mkutano huo wa CUF
na vyombo vya habari lakini baadae walipokea
taarifa ya kuahirisha kupisha ugeni wa Rais
Magufuli.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top