Taarifa ya Jeshi la kujenga (JWTZ) kuhusu chapicho la Gazet la Tanzania Daima septemba mosi.soma zaid
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na
gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari
4290 la tarehe 01 Septemba 2016, ikihusisha
shughuli za Jeshi hilo zinazoendelea katika
maadhimisho ya miaka 52 ya kuzaliwa
kwake na shughuli za kisiasa.
Tunapenda kuwataarifu wananchi
kwamba kazi ya Jeshi ni kulinda na
kutetea maslahi ya Taifa na mipaka ya
nchi, aidha, Jeshi letu linafanya kazi kwa
kufuata mila, desturi, nidhamu, kanuni na
sheria za Kijeshi kwa weledi wa hali ya
juu, hivyo lisihusishwe na propaganda
zozote za kisiasa kwani Jeshi letu ni lenye
maadili ya kitaasisi ya hali ya juu.
Jeshi ni taasisi ya dola wala si taasisi ya
kiitikadi, kwa maana uhusiano wake na
wanasiasa ni wakati linapotetea na
kulinda maslahi ya wananchi. Inaombwa
kuwa makini katika utoaji wa maelezo au
malalamiko, iachwe mara moja vyama
vya siasa kuingilia ratiba za Kijeshi.
Ikumbukwe kwamba tarehe 25 Julai kila
mwaka ni siku ya kuwakumbuka
Mashujaa wetu waliolitumikia Taifa hili
kwa umakini na nguvu zote kwa kuleta
mafanikio tunayoyaona, na hii ilipitishwa
mwaka 1979 wakati Majeshi yetu yanarudi
kutoka Uganda baada ya ushindi wa vita
vya Kagera.
Sherehe ya mapokezi hayo yalifanyika mji
wa Bunazi Wilaya ya Misenye wakati huo
Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera
ilipoanzishwa kuwa tarehe hiyo iwe siku
ya Mashujaa na kupitishwa Kisheria,
ikabaki siku ya tarehe 01 Septemba kuwa
ni siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania, hivyo jana
tulikuwa tunasherekea siku ya kuzaliwa
JWTZ. Ieleweke hivyo na iachwe mara
moja kuchanganya shughuli za Kijeshi na
mambo ya Kisiasa, viongozi wa kisiasa
wekeni kumbukumbu zenu vizuri.
Jeshi linasisitiza wanasiasa ni vizuri
wakasoma vema historia ya nchi
wanayotaka kuiongoza na wanayoongoza
ili kuepusha upotoshaji, lugha na maneno
yanayotolewa na viongozi wa kisiasa
wenye matakwa binafsi kuhusisha shughuli
za Jeshi na siasa zao yanatia ukakasi na
kiungulia, awe makini kuongea vitu
ambavyo haelewi na kutokuwa makini
zaidi aelewe madhara yanayoweza
kutokea kutokana na upotoshaji.
Jeshi letu linafanya shughuli zake ki
weredi.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na
Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.chanzo michuzi blog
0 comments :
Post a Comment