Mkurugenzi wa Yamoto bandi mkubwa Said Fella ameziweka hadharani nyumba tano za wasanii wake Yamoto Bandi.soma zaid
MKURUGENZI wa kituo cha Mkubwa na
Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani
nyumba takribani tano za wasanii wake
wa kundi la Yamoto Band na kuwataka
wananchi waelewe kuwa msanii anahitaji
nyumba na sio magari.
Nyumba hizo zilizojengwa nje ya mji
kidogo, Katika kata ya Kisewe amesema
kuwa hiyo ni moja ya maendeleo kwa
wasanii ,kwani hii si mara ya kwanza
kuwazawadia nyumba wasanii wake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es salaam, Fella amesema kuwa
ameamua kuziweka wazi hasa baada ya
kusikia maneno mengi kutoka kwa
wananchi wakidai kuwa Yamoto Band
hawafaidiki na Muziki wanaoufanya.
Fella amesema kuwa nyumba hizo mpaka
sasa hajajua thamani yake ila
zitakapokamilika ataita watu wa tathmini
kwa ajili ya kuziangalia ili kujua
zimetumika kiasi gani kwenye ujenzi huo.
Ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa
Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
kwa juhudi kubwa sana alizozifanya
katika kuhakikisha anafanikiwa kuinua
wasanii. Na katika nyumba hizo
zitakazozinduliwa hivi karibuni zitapatiwa
kwa Wasanii wanne wa Yamoto Band na
Mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma.
Meneja wa Mkubwa na Wanawe, Amani
Temba 'Mh. Temba' amesema kuwa hizi
nyumba zimejengwa kwa fedha za wasanii
wenyewe wanazozipata kwenye shoo za
muziki wanazozifanya na sio kama hela
zinazotoka mfukoni mwa kiongozi yoyote.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Twanga
Pepeta Asha Baraka amefurahishwa na
hatua hii kwani ni mara chache sana kwa
viongozi wa muziki kuchukua dhamana ya
kuwajengea nyumba vijana hawa wadogo
na amewataka wasanii kutokufanya
mzaha kwenye tasnia hii.
0 comments :
Post a Comment