Breaking News
Loading...

Advert

Friday, September 2, 2016

Majambazi yaua walinzi na kuteketeza mabweni.

Lushoto. Askari wa Kampuni ya Ulinzi ya Tele
Security ya Tanga, ameuawa kwa kupigwa risasi
na majambazi waliovamia Chuo Kikuu cha
Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (Sekomu)
wilayani hapa usiku wa kuamkia jana.
Majambazi hao ambao idadi yao inakadiriwa
kuwa kati ya 10 hadi 15, walivamia mabweni
mawili waliyokuwa wakilala wanafunzi
wasichana kisha kumwaga petroli katika
mabweni hayo na kulipua kwa kiberiti bweni
moja ambalo halikuwa na watu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,
Benedict Wakulyamba alisema tukio hilo lilitokea
saa tano usiku wa kuamkia jana katika mabweni
yaliyo jirani na ofisi kuu ya chuo hicho. Mlinzi
aliyeuawa ni Yohana Shemzigwa (34) na
mwenzake, Abuu Rajab (33) alijeruhiwa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top