Donard Trump amepoteza utajili $800m ya utajiri wake ndani ya mwaka mmoja.soma zaid
Mfanyabiashara tajiri wa New York anayewania
urais kupitia chama cha Republican nchini
Marekani Donald Trump amepoteza $800m ya
utajiri wake katika kipindi cha mwaka mmoja,
kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Jarida hilo linasema kwa sasa utajiri wa Bw
Trump ni $3.7bn (£2.7bn).
Forbes wanasema kushuka huko kwa thamani
ya utajiri wake kunatokana na 'kudorora kiasi'
kwa biashara ya nyumba na ardhi katika soko la
New York.
Bw Trump, ambaye wakati mmoja liandika
kitabu kwa jina Midas Touch (Mguso wa Midas:
Midas aliaminika kubadilisha kila alichogusa
kuwa dhahabu), amekuwa akisema kwamba rais
wa Marekani kwa sasa anaweza kuwa mtu
mwenye busara katika biashara na majadiliano.
Wakati wa mdahalo wa urais Jumatatu,
alisema: "Nina mapato makubwa ... wakati
umefika kwa taifa hili kuwa na mtu
anayefahamu mengi kuhusu pesa."
Mapema mwaka huu, hoteli mpya ya Trump
ilifunguliwa Washington DC, karibu na White
House
Alipoteza vipi $800m?
Forbes, ambao wamekuwa wakikadiria utajiri wa
Bw Trumo kwa zaidi ya miongo mitatu,
wanasema hilo limetokana na kudorora kwa
soko la nyumba, afisi na ardhi New York.
Kati ya majumba 28 ambayo yalichunguzwa na
Forbes, 18 yalishuka thamani, likiwemo jumba
maarufu la Trump Tower linalopatikana
Manhattan.
Jumba lake lililo 40 Wall Street na kilabu chake
cha Mar-a-Lago kilichopo Palm Beach, Florida,
pia vilipoteza thamani, kwa mujibu wa Forbes.
Lakini majumba saba ya Trump, likiwemo jumba
la pili kwa urefu San Francisco, yalipanda
thamani.
Ametumia pesa ngapi kwenye kampeni?
Inakadiriwa kwamba amewekeza $50m, pesa
zake binafsi, kwenye kampeni kufikia sasa.
Forbes wanakadiria kwamba matamshi yake
dhidi ya wahamiaji wa Mexico yalimgharimu $
100m kupitia mikataba aliyopoteza kwenye
mashirika makubwa kama vile NBC Universal,
Univision na Macy's.
Ivana na Donald Trump mwaka 1989
Utajiri wake kamili?
Utajiri wake kamili haujulikani. Alipowasilisha
taarifa zake za kifedha kwa Tume ya Dola ya
Uchaguzi, alisema ana "zaidi ya dola bilioni
kumi."
Lakini Forbes wanasema utajiri wake ni $3.7bn,
Bloomberg wanasema anamiliki $3bn nao
Fortune wanasema ana $3.9bn.
Moja ya sababu inayochangia hili ni kwamba Bw
Trump pia huhesabu thamani ya jina lake,
ambalo anakadiria kwamba thamani yake ni
karibu $3.3bn.
0 comments :
Post a Comment