Breaking News
Loading...

Advert

Monday, September 26, 2016

Majambazi yapora na kuua mtu mmoja mwanza.soma zaid

MTU mmoja amefariki dunia kwa kupigwa risasi
na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi
baada ya kuvamia na kupora kiasi cha fedha
ambacho hakijafahamika na simu nne za aina
mbalimbali katika duka la kuuza vifaa vya ujenzi
mtaa wa Nyakato Mecco Wilaya ya Ilemela
mkoani Mwanza.
Tukio hilo lilitokea jana saa 1:45 usiku ambapo
wavamizi hao ambao idadi yao haijajulikana
wakiwa na silaha aina ya SMG walivamia duka la
vifaa vya ujenzi mali ya Elikana Ngagaya na
kujaribu kupora maduka mengine ikiwa ni pamoja
na M-Pesa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed
Msangi, alimtaja aliyeuawa kuwa ni Grace Maega
(36) Mkazi wa Kangae ambaye alifariki muda
mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya
Bugando kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
“Inadaiwa wakati majambazi hao wanaondoka
eneo la tukio walifyatua risasi tatu zilizompata
kwenye bega la mkono wa kushoto wakati
akizima taa ndani ya duka lake lililopo jirani na
duka tajwa hapo juu kisha wakatokomea gizani.
“Majeruhi alikimbizwaHospitali ya Rufaa ya
Bugando kwa matibabu lakini alifariki dunia
masaa machache baadae kwa kuvuja damu
nyingi,” alisema.
Katika tukio hilo la unyang’anyi wa kutumia
silaha hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa
kuhusiana na mauaji hayo huku Jeshi la Polisi
likiendelea na msako pamoja na uchunguzi
kuhusiana na tukio hilo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini
hapo kwa ajili ya uchunguzi zaidi. “Tutafanya kila
tuwezalo kutumia ujuzi tulionao tukishirikiana na
wananchi kuhakikisha tunawakamata majambazi
hao.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top