Watendaji 3 wa kijiji wasimamishwa kazi wilayani Singida.soma zaid
WATENDAJI watatu wa vijiji katika wilayani ya
Manyoni mkoa wa Singida, wamesimamishwa
kazi kutokana na kushindwa kusimamia miradi
iliyopo kwenye vijiji vyao na kusababisha
upotevu wa fedha za serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa
wilaya hiyo, Geofrey Mwambe, alisema amefikia
hatua hiyo baada ya kutembelea vijiji hivyo
mwezi huu na kukutana na upotevu wa fedha
kwenye miradi mbalimbali ikiwamo ya maji huku
wengine wakiwa hawajui wajibu wao katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Aliwataja kuwa ni mtendaji wa kijiji cha Chikuyu,
Msemembo na Rungwa na kwamba pia
ameivunja kamati ya maji ya kijiji cha Chikuyu.
Alisema baadhi ya miradi hiyo ni wa maji wa
kijiji cha Chikuyu ambao mitambo yake inatumia
sola, lakini kwenye akaunti una Shilindimilioni
moja wakati mradi wa maji Soliya
unaoendeshwa mitambo ya aina hiyo, lakini una
zaidi ya Sh. milioni 40 kwenye akaunti.
Alisema watendaji hao hawawajibiki ipasavyo
kuisimamia miradi ya aina hiyo na kusababisha
serikali kupoteza mamilioni huku wengine
wakiendeleza vitendo vya rushwa.
Alisema viongozi watendaji katika wilaya hiyo
wasioendana na kauli ya Rais John Magufuli ya
“hapa kazi tu” ni bora wajitoe wenyewe ili
kupisha viongozi wawajibikaji wanaoweza
kuwajali wananchi kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumzia kuhusu maeneo ya wazi
yaliyovamiwa, Mwambe alisema mpango alionao
ni kuhakikisha maeneo yote ya umma
yanajengewa uzio na kuwekewa alama kwa
ulinzi zaidi.
“Maeneo ya umma yalivamiwa kutokana na
kutokuwapo kwa bikoni zinazoonyesha kuwa ni
mali za umma,” alisema.
Alisisitiza kama kuna kiongozi aliuza maeneo
hayo ya umma kwa watu binafsi, atachukuliwa
hatua za kisheria na kuirudisha mali ya umma.
0 comments :
Post a Comment